Home » » KALAMBO WATAHADHALISHWA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

KALAMBO WATAHADHALISHWA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

Mussa Mwangoka, Sumbawanga.

WANANCHI wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, wanaonufaika na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Sumbawanga hadi Bandari ya Kasanga wametahadhalishwa juu kuwepo kwa hatari ya kupata maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kutokana na ongezeko la watu katika maeneo hayo.

Mratibu wa tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania (TACAIDS) Mkoa wa Rukwa, Daniel Mwaiteleke alisema hayo jana wakati akizindua mradi wa kuelimisha wananchi kujikinga na maambukizi mapya ya ukimwi katika maeneo ambayo barabara hiyo inapita.

Mradi huo wa kuelimisha jamii unatekelezwa  na asasi ya Rukwa Society Servies Organization (RUSOSEO) ambapo ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye kata ya Kisumba Kasote kwa ufadhili wa kampuni ya uchimbaji madini Geita Gold Mining (GGM).

Mratibu huyo alisema kuwa wananchi wa maeneo hayo ambayo mradi huo wa barabara unatekelezwa wanakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa ni mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi hivyo wanapaswa kuwa makini kutokana na mwingiliano mkubwa wa wageni wanaoingia kufanya kazi katika kampuni hizo za ujenzi wa barabara kwani kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Alisema kinachotakiwa hivi sasa ni wadau ambao ni asasi za kiraia zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya ukimwi kwa kushirikiana na Serikali kuweka mikakati ya pamoja kwa kuanza kutoa elimu katika maeneo hayo ili kuinusuru jamii hiyo dhidi ya janga hilo.
“Afya za watu wetu ni za muhimu hivyo hatuna budi kulivalia njuga suala hilo ili kila mtu apate ufahamu wa kina juu ya suala la ukimwi na ipo haja ya kuwakumbusha mara kwa mara wapate kujua athari wanazoweza kupata iwapo hwatakuwa waangalifu” alisema Mwaiteleke.
Alisema kuwa mbali faida watakazopata wananchi wa maeneo hayo kijamii na kiuchumi kutokana na ujenzi wa barabra hiyo yenye urefu wa kilometa 112 ulitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2013 lakini itakuwa haina maana iwapo nguvu kazi iliypo itaangamia kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Naye, Mkurugenzi wa RUSOSEO, Dk Peter Lunyelele alisema kuwa licha ya taasisi hiyo kutumia wataalamu wenye uzoefu katika kutoa elimu ya kudhibiti maambukizi mapya ya ukimwi, pia wanatarajia kuzitumia kamati za kata na vijiji za kudhibiti ukimwi ili elimu hiyo iweze kuwafikia walengwa kama walivyokusudia.
 Blogzamikoa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa