Home » » WAWILI WAFA KATIKA TUKIO LA UJAMBAZI RUKWA

WAWILI WAFA KATIKA TUKIO LA UJAMBAZI RUKWA


Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa yetu blog

WATU wawili akiwamo mtu anayesadikiwa kuwa jambazi sugu wamefariki dunia katika kijiji cha Korongwe tarafa ya kabwe wilaya ya Nkasi mkoni Rukwa kufuatia kutokea tukio la uvamizi wa kutumia silaha.

Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema tukio hilo lilitokea jana usiku kwenye kijiji hicho baada watu watatu wanaodaiwa kuwa majambazi  walivamia nyumba ya mfanyabiashara mmoja aitwaye Regiusi Sembwe (26) ambaye inadaiwa walimpiga risasi na kumuua.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda, miongoni mwa watu hao wanaosadikiwa kuwa majambazi mmoja aitwaye Marijani Masumbuko (30) aliuawa na wananchi wenye hasira kali.

Inadaiwa kuwa baada ya watu hao kuvamia nyumba ya mfanyabiashara huyo walimkuta akiwa na rafiki zake ambapo walitaka wapewe fedha kitu ambacho kiliibua mzozo baina yao ndipo watuhumiwa hao wa ujambazi walipofyatua risasi iliyompiga kichwani Sembwe na kuanza kutokwa na damu nyingi kisha kufariki dunia muda mfupi baadaye.

Mwaruanda aliongeza kuwa wakati hali nikijitokeza watu hao walikimbia ambapo tayari wananchi wa kijiji hicho walikuwa wamefika eneo la tukio baada ya  kusikia milio ya risasi na kuanza kuwasaka majambazi hao ambapo walifanikiwa kumnasa mmoja wao na kuanza kumpiga kwa kutumia silaha mbalimbali za jadi zikiwamo Marungu, Mawe, Mapanga, Sime.

 Akielezea kwa kina, Kamanda huyo alisema kuwa baada ya kumpiga na kumjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo walianza jitihada za kumpeleka katika kituo cha afya lakini wakiwa njia alifariki dunia.

Hata hivyo alikuwa akiwa na bunduki aina ya SMG yenye risasi 26 ambayo alikuwa akiitumia kwa ajili kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo utekaji wa magari na wizi wa kutumia silaha ambapo alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu wa polisi mkoa wa Rukwa.


Kamanda Mwaruanda, alisema kuwa watuhumiwa wawili ambao walikimbia mara baada ya kutokea kwa tukio hilo wanaendelea kutafutwa na polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa