Mussa Mwangoka, Sumbawanga.(Rukwa yetu Blog)
MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Rukwa , Dk John Gurisha amewapiga marufuku tabia ya wakunga wa jadi mkoani humo kuzalisha akinamama na badala yake wawasaidie kuwafikisha katika vituo vinavyotoa huduma hiyo.
Dk Gurisha alitoa alisema hayo jana wakati akizungungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mijini hapa, ambapo alisema wakunga wa jadi wanaweza kuzalisha pale inapotokea dharura ambapo mama mjamzito anapopata uchungu wa ghafla lakini si vinginevyo.
“ Wakunga wa jadi nasema wasizalishe akina mama bali wawasaidie kuwafikisha katika vituo vya kutolea huduma ili waweze kupata huduma stahiki “ alisema .
Pia amewapiga marufuku madaktari na matabibu wanaotoa huduma katika hospitali na vituo vya afya vya umma mkoani humo kumwandikia mgonjwa dawa ambayo haipo ili aende kununua katika maduka ya madawa ya watu binafsi .
Alisema kuwa marufuku hiyo ni katika jitihadi za kuweka uthibiti wa madawa katika vituo vya umma vinavyotoa huduma ya afya mkoani humo pia kuwadhibiti madaktari na matabibu katika vituo hivyo kufanya hivyo ili wagonjwa walazimike kununua dawa katika maduka ya madawa ya binafsi ambayo baadhi ya maduka hayo yanamilikiwa na waoa wenyewe.
Alitahadharisha kuwa iwapo itabainika daktari ama tabibu amekiuka marufuku hiyo basi atachukuliwa hatua kali ya kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine wasiige tabia hiyo pia alibainisha kuwa Kamati ya Manunuzi ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ‘imekufa’ sasa imefufuliwa upya .
Hata hivyo alisema kuwa bado sekta hiyo ya afya mkoani humo bado inakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi wa afya wenye sifa katika kada zote zikiwemo za madaktari bingwa , madaktari , matabibu , wauguzi na wakunga .
0 comments:
Post a Comment