Home » » Sita wafa papo hapo katika ajali Sumbawanga

Sita wafa papo hapo katika ajali Sumbawanga


Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu Blog

WATU sita wamefariki dunia papo hapo na wengine 12 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiri nalo kuacha njia na kutumbukia mtoni katika barabara ya Sumbawanga - Mpanda.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, ajali hiyo ilitokea jana saa 7 mchana katika kijiji cha Ntendo nje kidogo ya Manispaa ya Sumbawanga na kulihusisha gari aina ya Fuso lenye Namba za usajili T 779 BTV lilokuwa likiendeshwa na Timotheo Matofali ambaye alitoroka baada ya kutokae ajali hiyo.

Alisema kuwa gari hilo lilikuwa likitoka katika kijiji cha Kisula kilichopo wilayani Nkasi na lilikuwa limebeba shena ya magunia ya mahindi ambapo inadaiwa lilishindwa kupata mlima kupinduka wakati likurudi nyuma na kutumbukia mtoni kwenye mto lukangao kusababisha vifo hivyo na majeruhi hao.

Kati ya watu sita waliofariki papo hapo ni maiti moja tu ndio iliyotambulika ambayo ni ya mwanamke aitwaye Iluminata Wampembe mkazi wa mjini Sumbawanga.

Kwa mujibu wa Mganga mkuu wa Manispaa ya Sumbawanga, Dk. Ally Mussa alisema kuwa kati ya watu sita waliofariki katika ajali hiyo wanne ni wanawake watu wazima, mtoto mmoja wa kike na mwanaume mmoja ambao wote majina yao hayajafahamika mara moja.

 Naye Mganga Mkuu wa hospitali ya Mkoa, Dk.Gasper Nduasinde aliwataja waliojeruhiwa na kulazwa katika namba tatu , tano na sita kuwa ni Vestus KIbandiko (35) mkazi wa Nkundi, Editha Hakimu (38), Getruda Sichilima (9), Severina Elimmani(38) wote wakazi wa Sumbawanga.

Wengine ni Ester Rupia mkazi wa Chanji, Queen Msukwa (47) Mkazi wa Chanji, Febroni Silapi mkazi wa

Katandala, Christina Mbaule (33) na mtoto wake Subesto Sinkala (1), Leorio Festo (40) MKazi wa majengo mjini hapa sambamba na mtoto mmoja ambaye jina lake halijafahamika mara moja.

“tumepokea majeruhi zaidi ya 20 lakini wengine wapatao nane waliokuwa na majeraha kidogo wamepata matibabu na kuruhusiwa kuondoka  huku 12 wakiwa wamelazwa hapa hospitalini wakiendelea na matibabu” alisema Dk. Nduasinde.

Kwa mujibu wa mmoja wa watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo, Kibandiko alisema kuwa gari hilo lilishindwa kupanda mlima hivyo kusimama kisha kuanza kurudi nyuma kwa kasi ka kutumbukia  mtoni.

“hilo gari lilibeba magunia ya mahindi…….kwa hiyo magunia hayo yalitukandamiza na ndio yamechangia watu wengine kufariki dunia papo hapo kutokana na kukandamizwa huko” alisema.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa