Home » » Miss Redd's kwa mkoa wa Rukwa kufanyika Kesho, wajiandaa vizuri.

Miss Redd's kwa mkoa wa Rukwa kufanyika Kesho, wajiandaa vizuri.

 Washiriki wa shindano la Redd's Miss Rukwa 2012 wakiwa katika mazoezi ya kujiandaa kwaajili ya  kinyang'anyiro hicho kitakachofanyika kesho katika ukumbi wa Bomani mjini Sumbawanga. Picha na Mussa Mwangoka
 Mmoja wa warembo wanaoshiriki kwenye kinyang'anyiro hicho kitakachofanyika leo katika ukumbi wa Bomani mjini Sumbawanga, Vency Edward akizizungumza na waandishi wa habari namna alivyojiandaa kutwaa taji hilo. Picha na Mussa Mwangoka


Muaandaji wa Shindano la Redd's Miss Rukwa 2012, Mariam Amri Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa mazoezi ya washiriki wa kinyang'anyiro hicho kitakachofanyika kesho katika ukumbi wa Bomani mjini Sumbawanga. Picha na Mussa Mwangoka


Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa yetu

SHINDANO la kumsaka Mrembo wa mkoa wa Rukwa yajulikanayo kama  Redd’s miss Rukwa 2012 litafanyika kesho June 30 katika ukumbi wa Bomani uliopo mjini Sumbawanga.

Waandaji wa shindano hilo kampuni ya Fantastic Entertainment$Promotion wamedai kuwa asilimia kubwa ya maandalizi ya shindano hilo yamekamilika na kinachosubiliwa ni kumpata mrembo wa Mkoa huo atakaye shiriki katika shindano la Redd’s miss Tanzania 2012.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika kambi ya mazoezi ya warembo wanaotarajiwa kushiriki katika kinyang’anyiro hicho, mkurugenzi wa kampuni hiyo Mariam Amri alisema anawashukuru wale wote ambao wameshiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha shindano la mwaka huu.

Alisema kuwa mpaka sasa warembo 10 wamejitokeza kushiriki katika shindano hilo na wapo kambini na wakiendelea na mazoezi kwa ajili ya kinyang'anyiro hicho ambapo wapo chini ya msimamizi wa mazoezi hayo Miss Rukwa 2011 Atu Daniel ambaye kazi yake kubwa ni kuhakikisha warembo watakaoshiriki shindano la Redd’s miss Rukwa 2012 wanafanya vizuri.

Mariam Aliwataja warembo hao kuwa ni Vency Edward, Joketi Joseph, Hawa Abbas, Asia Abdallah, Rosemary Emmanuel, Salma Hilali, Slivia Emmanuel, Angela Joseph, Jackline Godfrey na Anganile Rodgers,  

Aliwataja watu waliojitokeza kudahamini shindano hilo kuwa ni chuo cha Musoma Utalii collage,Kampuni ya Zuku TV, Minah Restaurant, Kiluswa Hardware, Villa Restaurant na Mwandele The Best Communication, huku wasanii wataotumbuiza ni pamoja na Mkali wa muziku wa kizazi kipya Timbulo anayewika kibao cha domo langu atakayesindikizwa na Bendi ya Mtipemtipe ya mjini hapa.

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa