Home » » MKUTANO WA WADAU WA NHIF MKOANI RUKWA KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 10 YA UTOAJI HUDUMA NCHINI

MKUTANO WA WADAU WA NHIF MKOANI RUKWA KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 10 YA UTOAJI HUDUMA NCHINI


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia wadau wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoani Rukwa katika ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga. Katika hotuba yake hiyo aliutaka mfuko kuboresha huduma zake mara kwa mara na kuhakikisha wanawafikia wananchi wengi zaidi kujenga uelewa wa mfuko na faida zake ili waweze kujiunga. Aidha aliutaka mfuko kushughulikia malalamiko yote yanayotolea na wadau juu ya huduma zinazotokana na mfuko kwa ustawi wa mfuko na jamii kwa ujumla. Mfuko wa Bima ya Afya nchini unaadhimisha miaka 10 ya kujituma na kuaminiwa ambapo kaulimbiu yake ni "Huduma za matibabu vijijini na huduma bora za afya kwa wote.   
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Injinia Stella Manyanya (katikati) akizungumza na wadau wa mfuko wa NHIF katika ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga. Kulia ni Mganga Mkuu Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Gurisha John William, Afisa Tawala Mkoa wa Rukwa Festo Chonya, Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Mkoa wa Katavi Lauteny Kanoni, Mjumbe wa Bodi ya NHIF, Naibu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Bima ya Afya Nchini Hamis Mdee na Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini Ndugu Hamis Mdee akizungumza kwenye mkutano huo. Alisema lengo kubwa la kufanya ziara Mkoani Rukwa ni kutoa taarifa za mfuko wa bima ya afya na mfuko wa afya ya jamii pamoja na kuelezea umuhimu wa mifuko hiyo kuhamasisha jamii kujiunga ili kuongeza ushiriki katika mifuko hiyo.
Wataalamu wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini ambao walikuwa Sekretarieti ya kikao hicho wakiwa kazini.
Wadau wa Mfuko wakifuatilia mada mbalimbali katika kikao hicho.
Picha ya pamoja kati ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, viongozi wa mfuko wa bima ya afya ya jamii nchini, na wadau wa mfuko huo.
Picha ya pamoja. Timu ya viongozi na wataalamu wa mfuko wa bima ya afya nchini wameondoka leo kuelekea Kata ya Chala iliyopo Wilayani Nkasi kwa ajili kuwapa wananchi elimu ya msingi juu ya mfuko na kuwahamasisha kujiunga.
Picha na OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa