Home » » Matumizi ya mbegu zisizo na ubora ni chanzo cha mavuno duni

Matumizi ya mbegu zisizo na ubora ni chanzo cha mavuno duni

 Mkuu wa mradi wa utafiti wa mbegu bora za Maharage, Michael Kilango kutoka kituo cha ufatifi cha Uyole mkoani Mbeyaakitoa elimu kwa wananchi kuhusu uzalishaji wa mazao ya maharage kwa kutumia mgegu bora za 04 leo katika kijiji cha Milundikwa kilichpo wilayani Nkasi.

  Mkuu wa mradi wa utafiti wa mbegu bora za Maharage, Michael Kilango kutoka kituo cha ufatifi cha Uyole mkoani Mbeya akitoa maelezo kwa wananchi wa kijiji cha Milundikwa leo kuhusu matumizi ya mbegu bora huku wakiwa ameshika aina ya mbegu ilifanyiwa utafiti na kuonekana inafaa iitwayo Uyole 04.
 Wakazi wa vijiji vya Milundikwa, Malongwe, Kisula na Kasu wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa wataalamu wa kilimo kutoka kituo cha utafiti wa mbegu ch Uyole (hawapo pichani) leo nje ya kituo cha habari za kilimo kilichpo Milundikwa. Picha zote na Mussa Mwangoka.

****************
Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Ruvuma yetu

IMEELEZWA kuwa tabia iliyojengeka miongoni mwa baadhi ya wakulima wa mazao ya maharage wilayani Nkasi mkoani Rukwa ya kutumia mbegu zisizo na ubora ni miongoni mwa sababu zinazochangia uzalishaji wa mazao yao kuwa chini.

Mkuu wa mradi wa utafiti wa mbegu bora maharage,kutoka kituo cha utafiti wa mbegu kilichopo Uyole mkoani mbeya, Michael Kilango alisema hayo leo wakati akizingumza na wakulima wa vijiji vya Milundikwa, Kasu, Malongwe na Kisula baada ya kutembelea mashamba ya utafiti mbegu bora za maharage aina ya 04 yaliyopo katika kijiji cha Milundikwa wilayani humo.

Alisema wakulima wengi wa mazao hayo wamejenga utamaduni wa kutumia mbegu za asili ambazo hazina ubora hivyo kufanya uzalishaji kutokuwa na tija ukilingansha na ukumbwa wa eneo wanalotumia kwenye shughuli hiyo.

Kilango alisema kuwa imefika wakati sasa wakulima hao wanapaswa kubadilika kifra na mtazamo kwa kuanza kutumia mbegu bora na zilizofanyiwa utafiti wa kina na wataalamu kutoka katika kituo cha utafiti ambao wamejikita kwenye maeneo ya vijijini kwa lengo la kuwasaidia wakulima.

"kwa mfano ukitumia mbegu maharage ya 04 ambayo tumeifanyia utafiti na kuona inafaa kwa maeneo ya wilaya ya Nkasi mkulima atapata manufaa makubwa kwa kuwa katika ekari moja anapata wastani wa gunia nane" alisema Kilango.

Aliongeza kuwa Mradi wa utafiti wa mbegu bora za maharage unafanywa katika wilaya nne za Chunya (Mbeya), Iringa vijijini (Iringa), Nkasi (Rukwa) na Mpanda mkoani Katavi ambapo pamoja na kuwepo kwa mashamba ya utafiti pia timu ya wataalamu wa kutoka kituo cha utafiti cha Uyole utoa elimu na kuwahamasisha wakulima kutumia mbegu zilizofanyiwa utafiti na kituo hicho.Matumizi ya mbegu zisizo na ubora ni chanzo cha mavuno duni

Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Mtwara yetu

IMEELEZWA kuwa tabia iliyojengeka miongoni mwa baadhi ya wakulima wa mazao ya maharage wilayani Nkasi mkoani Rukwa ya kutumia mbegu zisizo na ubora ni miongoni mwa sababu zinazochangia uzalishaji wa mazao yao kuwa chini.

Mkuu wa mradi wa utafiti wa mbegu bora maharage,kutoka kituo cha utafiti wa mbegu kilichopo Uyole mkoani mbeya, Michael Kilango alisema hayo leo wakati akizingumza na wakulima wa vijiji vya Milundikwa, Kasu, Malongwe na Kisula baada ya kutembelea mashamba ya utafiti mbegu bora za maharage aina ya 04 yaliyopo katika kijiji cha Milundikwa wilayani humo.

Alisema wakulima wengi wa mazao hayo wamejenga utamaduni wa kutumia mbegu za asili ambazo hazina ubora hivyo kufanya uzalishaji kutokuwa na tija ukilingansha na ukumbwa wa eneo wanalotumia kwenye shughuli hiyo.

Kilango alisema kuwa imefika wakati sasa wakulima hao wanapaswa kubadilika kifra na mtazamo kwa kuanza kutumia mbegu bora na zilizofanyiwa utafiti wa kina na wataalamu kutoka katika kituo cha utafiti ambao wamejikita kwenye maeneo ya vijijini kwa lengo la kuwasaidia wakulima.

"kwa mfano ukitumia mbegu maharage ya 04 ambayo tumeifanyia utafiti na kuona inafaa kwa maeneo ya wilaya ya Nkasi mkulima atapata manufaa makubwa kwa kuwa katika ekari moja anapata wastani wa gunia nane" alisema Kilango.

Aliongeza kuwa Mradi wa utafiti wa mbegu bora za maharage unafanywa katika wilaya nne za Chunya (Mbeya), Iringa vijijini (Iringa), Nkasi (Rukwa) na Mpanda mkoani Katavi ambapo pamoja na kuwepo kwa mashamba ya utafiti pia timu ya wataalamu wa kutoka kituo cha utafiti cha Uyole utoa elimu na kuwahamasisha wakulima kutumia mbegu zilizofanyiwa utafiti na kituo hicho.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa