Home » » MKUU WA MKOA WA RUKWA AANZISHA MPANGO WA RUKWA SALAMA UTAKAOHUSISHA UJENZI WA NYUMBA BORA ZA MAKAZI YA ASKARI POLISI MKAOANI HUMO JANA

MKUU WA MKOA WA RUKWA AANZISHA MPANGO WA RUKWA SALAMA UTAKAOHUSISHA UJENZI WA NYUMBA BORA ZA MAKAZI YA ASKARI POLISI MKAOANI HUMO JANA


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa (RPC) Sunto
Mantage wakiimba wimbo wa Utii wa Jeshi la Polisi kabla ya Mkuu huyo wa Mkoa
kuzungumza na Polisi jana. Lengo la Mkuu huyo wa Mkoa kukutana na Jeshi
hilo ilikuwa ni kujadili juu ya azma yake ya kuboresha makazi ya nyumba za
Polisi Mkoani humo. Alisema kuwa kuna uhaba mkubwa wa nyumba za Polisi na hata
zilizopo sio muafaka sana. Katika mpango huo maoni mbalimbali yalitolewa ikiwemo
Polisi wenyewe kujitolea nguvu kazi kwa kufyatua matofali na michango kabla ya
kuwashirikisha wadau wengine katika kuchangia zoezi hilo. Aidha Mkuu huyo wa
Mkoa alisema kuwa alionana na Waziri wa Mambo ya ndani na kumueleza tatizo
lililopo ambapo aliahidi kutoa ushirikiano na Mkoa katika zoezi hilo. Katika
kuhakikisha zoezi hilo linaaanza mara moja Injinia Manyanya alitoa ahadi ya
kuchangia shilingi milioni 3.5. Alisema kuwa mapambao dhidi ya uhalifu na Rukwa
kuwa salama hayawezekani bila Polisi wenyewe kuwa salama na kwamba hicho ndicho
kilichomsuukuma kuanzisha mpango huo wa ujenzi wa makazi ya nyumba bora za
Polisi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Injinia Stella Manyanya akizungumza na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa
jana ambapo alitangaza rasmi mpango wa Rukwa salama. Katika mazungumzo hayo
aliwataka askari wote kuwa na moyo wa kizalendo kwa kuipenda nchi yao na
Serikali kwa ujumla. Aliwataka waache kasumba ya kuichukulia Serikali yote kuwa
ni mafisadi pale mtu mmoja anapohusika na tukio hilo, kwani hata wao wenyewe
kama Serikali wanapambana na ufisadi kwa maslahi ya nchi. Kuhusiana na mchakato
wa mabadiliko ya katiba aliwataka Polisi washiriki kikamilifu katika mchakato
huo kuhakikisha wanaingiza vipengele muhimu vinavyohusu jeshi hilo na kuondoa
vile vyenye mapungufu. Pia aliwataka Polisi wazihamasishe familia zao na wao
wenyewe washiriki katika zoezi lijalo la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika
nchini kote tarehe 26 Agosti 2012.
Sajenti Bahati
akionyesha vifaa hivyo kwa Wapiganaji wenzake. Alimshukuru Mkuu huyo wa Mkoa na
kusema kuwa yeye ni Kiongozi wa mfano kwani hawajawahi kuona Mkuu wa Mkoa
kuzungumza na Jeshi la Polisi hapo awali katika Mkoa wa
Rukwa.
Baadhi ya Askari
Polisi walioshiriki katika Kikao hicho wakifuatilia kwa umakini majadiliano
yaliyokuwa yakiendelea.

(Picha zote na rukwareview.blogspot.com)
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa