POLISI mkoani Rukwa inamshikilia mwalimu wa Shule ya Sekondari
Miangalua iliyopo katika wilaya ya Sumbawanga akituhumiwa kumpatia
ujauzito mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 16, ambaye alikuwa akisoma
kidato cha tatu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kuwapo
kwa tukio hilo, akisema tayari mtuhumiwa huyo amekamatwa na anashikiliwa
kwa mahojiano na katika Kituo cha Polisi kilichopo katika mji mdogo wa
Laela wilayani Sumbawanga.
Atafikishwa mahakamani mara tu baada ya upelelezi wa awali kukamilika
ambapo anatuhumiwa kwa makosa matatu ya kumpatia ujauzito mwanafunzi
huo, kumbaka na kukatisha masomo yake.
Akizungumzia mkasa huo, Mkuu wa shule hiyo, Gishi Milundi amekiri
kutokea kwa mkasa huo ambapo mwalimu wake anahusishwa na tuhuma hizo
huku akiongeza kuwa, baada ya kuhisiwa kuwa ana dalili za ujauzito
alikwenda kupimwa katika zahanati ya Miangalua na kubainika kuwa na
ujauzito wa miezi mitano.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment