Home » » MWALIMU MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMPA MWANAFUNZI MIMBA

MWALIMU MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMPA MWANAFUNZI MIMBA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Imeandikwa na Pety Siyame, Sumbawanga
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia mwalimu wa Shule ya Sekondari Miangalua iliyopo katika wilaya ya Sumbawanga akituhumiwa kumpatia ujauzito mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 16, ambaye alikuwa akisoma kidato cha tatu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo, akisema tayari mtuhumiwa huyo amekamatwa na anashikiliwa kwa mahojiano na katika Kituo cha Polisi kilichopo katika mji mdogo wa Laela wilayani Sumbawanga.
Atafikishwa mahakamani mara tu baada ya upelelezi wa awali kukamilika ambapo anatuhumiwa kwa makosa matatu ya kumpatia ujauzito mwanafunzi huo, kumbaka na kukatisha masomo yake.
Akizungumzia mkasa huo, Mkuu wa shule hiyo, Gishi Milundi amekiri kutokea kwa mkasa huo ambapo mwalimu wake anahusishwa na tuhuma hizo huku akiongeza kuwa, baada ya kuhisiwa kuwa ana dalili za ujauzito alikwenda kupimwa katika zahanati ya Miangalua na kubainika kuwa na ujauzito wa miezi mitano.
CHANZO HABARI LEO
 
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa