Na
Walter Mguluchuma , Sumbawanga-Rukwa yetu
WATU
8 wanadhaniwa kufa maji katika ziwa Tanganyika baada ya boti waliyokuwa
wakisafiria kutokea kata ya Kirando kwenda Korongwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa
kugongana na boti ya wavuvi waliokuwa wanakwenda kuvua samaki ambapo boti ya
abiria ilipasuka na kuzama majini.
Taarifa
iliyotolewa na mkuu wa wilaya Nkasi Idd Hassan Kimanta ilisema kuwa tukio hilo
lilitokea usiku wa tarehe 7 mwezi huu majira ya saa 3 za usiku ambapo baada ya boti
hizo kugongana boti la abiria lilizama na boti la wavuvi lililofanya tukio hilo
walikimbia hadi boti nyingine iliyokua majini humo ilipokuja kuwakoa.
Alisema
baada ya hilo serikali wilayani Nkasi ilichukua hatua za kuanza kuwasaka watu
waliodhaniwa kuwa wamekufa maji siku nzima lakini mpaka sasa hakuna mwili
wowote wa marehemu uliokutwa majini na kuwa wanasubiri sasa miili hiyo pale
itakapoanza kuelea majini na ndipo waokoaji watakapoanza kuiopoa miili hiyo
Alidai
kuwa kati ya watu 8 wanaodhaniwa kufa maji kati yao watano ni watu wazima
ambapo wanaume ni watatu na wanawake ni wawili,na watoto waliofia katika ziwa
hilo ni watatu.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema kuwa wanadhania watu hao kufia majini baada ya
ajali hiyo kutokea na wao hawaonekani tena licha ya kuwa miili yao haionekani
na ndiyo maana kuna jitihada ambazo serikali inazifanya za kuitafuta miili hiyo
yote na kuwa zoezi hilo likikamilika ukweli halisi wa watu waliofia majini
utabainika na huenda idadi ikaongezeka zaidi.
Awali
afisa mtendaji wa kata ya Korongwe Rock Msalange alimwambia mkuu wa wilaya kuwa
baada ya ajali hiyo kutokea na zoezi la kuwakoa abiria waliokuwemo katika boti
ya abiria kukamilika waliamua kuwakamata madereva wa boti zote hizo mbili na
kuwakabidhi polisi kwa hatua zaidi za kisheria.
Aliwataja
madereva wa maboti hayo kuwa ni Stephano Abbas (34) aliyekua akiendesha boti la
abiria ikiwa ni pamoja na madereva wawili wa boti la wavuvi ambao ndiyo
waliosababisha ajali hiyo ambao ni Approtas Ronati (33) na Gervas Pesambambili (31)
ambao bado wanashikiliwa na jeshi la Polisi.
Baadhi
ya Wahanga wa tukio hilo walionusurika Korastika Boaz ambaye amempoteza mtoto
wake wa kiume wa miaka 6 katika ajali hiyo alisema kuwa ajali hiyo baada ya
kutokea yeye alikua na watoto wawili katika boti hiyo na vitu mbalimbali lakini
alipatwa na bumbuwazi na kushindwa kumokoa mtoto wake huyo ambaye amefia majini
ikiwa ni pamoja na vitu vyake vyote vimepotea katika ziwa hilo
0 comments:
Post a Comment