Home » » HATARI: BIASHARA YA NGONO HATARI MKOANI RUKWA

HATARI: BIASHARA YA NGONO HATARI MKOANI RUKWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 WALTER MGULUCHUMA.
Sumbawanga.

KASI kubwa ya ongezeko la wageni wanaoingia na kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi katika mkoa wa Rukwa, imetajwa kwamba ndio kiini cha kushamiri kwa biashara ya ngono hivyo kusababisha kuongezeka kwa kasi kubwa ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa ukimwi.

Mkurugenzi wa Shirika la lisilo la Kiserikali  la Resource Oriented Development  Initiative (RODI), Gideon Mpina alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya kupambana na maambukizi ya VVU na kutoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia (TMEP) inayotekelezwa na asasi ya Rodi kwa ufadhili wa taasisi Elimu  ya Afya na Uzazi cha nchini Sweden (RFSU)

Waandishi hao waliotaka kujua sababu za kuongezeka kwa kasi kubwa kwa maambuziki ya VVU yaliyofikia asilimia 6.2 kutoka 4.9 kwa kipindi cha miaka mitatu hadi sasa wakati zipo taasisi nyingi zisizo za kiserikali (NGOs) zimejikita kwenye eneo hilo kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya maradhi hayo.

Mpina miradi  alisema kwamba wageni wengi wanaoingia kwenye mkoa huo kwa lengo la kufanya shughuli za kiuchumi ikiwa ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, ununuzi wa mazao na uvuvi wamekuwa wakitumia fedha nyingi kufanya anasa hivyo kuchochea biashara ya ngono pasipo matumizi ya kondomu.

"Kasi hii ya maambukizi ya virusi vya ukimwi imetokana na ongezeko la wageni hawa ambao ni wafanyakazi wa kampuni za ujenzi wa barabara, wavuvi kwenye kambi zao katika ziwa Rukwa  na wanunuzi wa mazao  huko ndio kunafanyika sana ngono zembe, watu hawajali kabisa matumizi ya kondomu" alisema Mpina

Aliongeza kuwa ili kudhibiti hali hiyo bado jitihada za makusudi zinahitajika kufanya na wadau wa ukimwi ikiwemo Rodi ambapo kupitia miradi wake wa TEMP wataendelea kutoa elimu, kuhamasisha matumizi ya kondomu na watu kupima ili kujua afya zao hali ambayo itasaidia kupunguza kasi ya maambukizi hayo.

Kwa upande wake, Mratibu wa TEMP mkoa, Dk John Komba alisema kuwa elimu ya afya ya uzazi imesaidia sana kupunguza matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, ushiriki wa  wanaumekatika afya ya uzazi umekuwa mkubwa kwani wengi  wamekuwa na mwamko wa kuwasindikiza wake zao kliniki kabla na baada ya kujifungua hali.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa