Home » » MZEE WA MIAKA 97 AFANYA TAMBIKO ILI MKEWE ASHIKE MIMBA NA KUZAA MTOTO WILAYANI NKASI.

MZEE WA MIAKA 97 AFANYA TAMBIKO ILI MKEWE ASHIKE MIMBA NA KUZAA MTOTO WILAYANI NKASI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mathias Kisokota.

BABU aliyefunga ndoa mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka 94, Mathias Kisokota mkazi wa Kitongoji cha Isunta, Namanyere wilayani Nkasi ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 97, amehamia na mkewe katika Mji wa Mpulungu mwambao wa Ziwa Tanganyika nchi jirani ya Zambia miezi sita iliyopita kwa lengo la kufanya tambiko la kumwezesha mkewe mwenye umri wa miaka 83 kupata mtoto wa uzeeni.

Mke wa mzee huyo, Uria Mwamanzi ni mwenyeji wa nchi jirani ya Zambia alizaliwa na kukulia katika Mji wa Mpulungu mwambao mwa Ziwa Tanganyika ambapo kwa mujibu wa wajukuu zao ndiko babu yao alipokutana naye na kuwa na mahusiano hadi walipofunga ndoa miaka mitatu iliyopita.

Wanandoa hao ambao waliacha gumzo kubwa baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Anthony, alasiri ya Juni 18, 2011 mjini Namanyere Makao Makuu ya Wilaya ya Nkasi.

Akizungumza na mwandishi wa habari kwa njia ya simu kutoka katika Mji wa Namanyere jana, Salvatory Adolf (19), mjukuu wa wazee hao kutoka kwa mtoto wao kitindamimba mwenye umri wa miaka 40 sasa, alisema babu yake amemsindikiza mkewe huyo ili kwenda kutambikia mizimu ya kwao.

“Bibi hakuwa na raha mara kwa mara alikuwa akitamani kurudi nchini kwao Zambia kuwasalimia nduguze pia akiwa huku alikuwa akiugua mara kwa mara hivyo babu aliona bora amsindikize bibi akatambike kwa mizimu ya babu zake nchini humo,” alisema.

Hata hivyo, hakutaka kueleza kwa undani juu ya kiu ya babu yake ya kutaka kupata mtoto, habari ambazo zinazungumzwa na watu wa karibu waliopo ndani ya familia ya wanandoa hao.

Miongoni mwao, Agnes ambaye ni mtoto wa mwisho wa Mzee Kisokota akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutoka mjini Namanyere, Nkasi alisema baba yake amekuwa na hamu hadi sasa ya kupata mtoto katika ndoa yake changa. “Anasali sana akiomba kila siku apate mtoto katika ndoa yake.

Bado ana matumaini makubwa ….. nikianza kukusimulia tutakesha, tena anasema siku akijaliwa mtoto katika ndoa yake hiyo atajawa na furaha kubwa na kufanya sherehe ya aina yake… amemsindikiza bibi (mkewe) Zambia kusalimia ndugu zake pia kutambika kwa kuwa baba ana hamu ya mtoto atatumia fursa hii nae kutambikia kwa wakwe zake ili mkewe huyo ashike mimba,“ alieleza Agnes.

Hali hiyo inakuja licha ya ukweli kwamba, umri wa mke wa Mzee Kisokoto kuzaa umeshapitiliza, lakini kwa pamoja wamedaiwa kuamini kwa Mungu hakuna kisichowezekana hivyo anaweza kutenda miujiza kwa kuwapa baraka ya mtoto wa ndoa yao ya uzeeni.

Mjukuu huyo alipoulizwa juu ya ziara hiyo kuhusisha pia kusaka mtoto kutoka kwa `mizimu’ ya ukoo wa mke wa babu yake, hakuwa na majibu ya moja kwa moja.

“Bibi alipoondoka alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mwili lakini tangu atambike nchini Zambia inadaiwa amepona kabisa na sasa wanaishi raha mustarehe na babu… ila watarudi huku kwetu baadae mwaka huu …”, alisema.

Katika safari ya wazee hao, Adolf anasema bibi na babu yake walisindikizwa na Claudio Mathias (21), kaka wa mjukuu huyo na kwamba kaka huyo amesharejea nchini.

Wanandoa hao kwa mujibu wa wajukuu zao kabla ya kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga mjini Namanyere miaka mitatu iliyopita walikuwa wakiishi ‘kinyumba’ kila mmoja wao akibahatika kuwa na watoto katika mahusiano yake ya awali.

Kwa pamoja wana wajukuu zaidi ya 30 na vitukuu zaidi ya 40 wengi wao wakiishi nchi jirani ya Zambia. Mzee Kisokoto alifiwa na mke wa kwanza zaidi 
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa