Home » » UKOSEFU WA DAWA KATIKA VITUO VYA AFYA WAKWAMISHA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA MSINGI

UKOSEFU WA DAWA KATIKA VITUO VYA AFYA WAKWAMISHA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA MSINGI

Na Walter Mguluchuma.
Nkasi

UMASIKINI uliokithiri miongoni mwa wakazi wa wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa na ukosefu wa vifaa tiba zikiwemo dawa ni katika vituo vinavyotoa huduma za afya vimetajwa ni sababu kubwa zinazochangia wananchi wasihamasike kujiunga na mfuko wa afya ya msingi (CHF) wilayani humo.


Mkuu wa wilaya ya Nkasi, Iddy Kimanta alisema hayo jana ofisi kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wanatembelea mradi wa wazazi na mwana unaotekelezwa na mashirika ya Africare, Jhpiego na Plan International.

Mradi huo unatekelezwa katika wilaya ya Nkasi, Kalambo na Sumbawanga vijijini na unalenga kuboresha huduma za afya na kupunguza tatizo la vifo vya akinamana wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa pamoja na serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa afya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo lakini mwamko umekuwa hafifu kutokana na umasikini wa kipato unaowakabili wakazi wa wilaya hiyo.


Ambapo Pato la wananchi mmoja katika wilaya hiyo ni wastani
wa Sh 560,000 kwa mwaka lakini pia vituo vingi vya afya kutoa huduma ambazo haziridhishi.

"Mtu kupata Sh 10000 ya kujiunga kwenye mfuko huo ni kazi kubwa lakini waliobahatika kujiunga wanaeleza wazi kwamba huduma zinazopatikana kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ni hafifu na haziridhishi hata kidogo, hakuna dawa na vifaa tiba vingine kwa hiyo hamasa inakwisha kwa wengine" alisema Kimanta.

Aliongeza tatizo bado lipo kwa bohari ya madawa (MSD) wanachelewa kufikisha dawa kwa wakati kwenye vituo vya afya mathalani maombi yanachukua zaidi ya miezi mitatu hadi sita ndio dawa ziwafike kwenye vituo vyenye mahitaji.

Pia mkuu huyo wa wilaya alitaja sababu nyingine ya ukosefu vifaa tiba vya kutosha kwenye vituo vingi vinavyotoa huduma ya afya hususani mwambao wa ziwa Tanganyika ni wageni wengi kutoka nchi jirani ikiwemo Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo (DRC) kukimbilia kwenye vituo hivyo kupata huduma za kiafya hivyo vituo kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa kuliko uwezo wake.

"Wageni wengi sana unaweza kupita katika kituo kimoja cha afya ukakuta idadi kubwa ya wagonjwa waliolazwa ni wageni kwa hiyo lazima dawa na vifaa vingine viishe kwa haraka kuliko muda uliopangwa maana mahitaji ni makubwa mno"alisema Kimanta.

Alisema kwamba pamoja na changmoto hizo serikali inaendelea na jitihada za kuboresha hudama ya afya kwa kuhamasisha wananchi wajiunge na mfuko huo sambamba kuhakikisha mahitaji mengine kama dawa yanafika kwa wakati kutoka
bohari ya dawa (MSD).

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

1 comments:

Anonymous said...

Tunaomba uwe unatuwekea tarehe,mwezi na mwaka tukio lilipo tokea ili iwe rahisi kufuatilia habari.
Nawatakia uhabarishaji mwema

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa