Home » » JESHI LA POLISI LATOA MAJINA YA WATU WALIOFARIKI KATIKA AJALI MKOANI RUKWA

JESHI LA POLISI LATOA MAJINA YA WATU WALIOFARIKI KATIKA AJALI MKOANI RUKWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Walter  Mguluchuma    Na  Irene  Temu
Nkasi
JESHI la polisi mkoani Rukwa limetoa majina ya watu waliofariki katika ajali ya Fuso lenye namba za usajili T425 BFF ili ndugu zao wakachukue miili ya marehemu kwaajili ya kwenda kufanya maziko.   

Kamanda wa polisi mkoani humo Georege  Kyando alisema kuwa miili ya watu waliokufa katikaajali hiyo  ni wanawake 10 nawanaume watano huku baadhi ya ipo katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Nkasi. 

Aliwataja marehemu hao kuwa ni Domona Tenganamba(41),Emaanuel Rashif(84),Restuta Sunga(35) Salula Revena(38)FeresiaTenganamba(12)
Prisca Madeni(45).

Aliwataja wengine kuwa ni mwalimu washuleya msingi Kalambanzite,  Richard Chikwangara(24)Yusta Somambuto(36),Giles Ramadhani(24),
Odetha Madirisha(46)Megi Nalunguli(52)

Kamanda Kyando Aliwataja wengine kuwa ni Abuu Amani Mandevu(37)Nyandindi Batrahamu(35) Magdalena Mbalamwezi(50) pamoja na mtoto mwenye umri wa wiki mbili ambaye bado hajapewa Jina.

Pia aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Dismas Clement(26),Sema Savery(25)Ally Haruna(33),Yusta Mfundimwa(50)Tenesfory Oscar(36) Amos Kitambale(25) Neema Mwanandenje(21)Joseph Sungula(28) namwanamke mmoja ambaye Yupo chumba cha wagonjwa mahututi I. C. U na hajafahamika jina lake mpaka sasa. 

Alisema kuwa marehemu na majeruhi wa ajari hiyo ni watu kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini ni vizuri wananchi wakafuatilia ili kujua kama kuna ndugu yao wafanye mawasiliano kwani serikali iliahidi kusafirisha maiti mpaka watakapofanya maziko.

Alisema kuwa dereva wa gari hilo bado anasakwa na atakapopatikana afikishwe mbele ya sheria kwa uzembe nakusababisha ajali iliyo sababisha vifo hivyo. 

Naye mkuu wa wilaya  ya Nkasi Said Mtanda alimshukuru rais John Magufuli kwa kuungana na wafiwa wote katika katika kipindi hiki cha majonzi kwa kuondokewa na ndugu zao kwa ajali mbaya ya gari.
 

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa