Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin
Ngonyani akijibu hoja toka kwa Wabunge mbalimbali katika cha 7 cha Bunge
la 11 linaloendelea Mjini Dodoma. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
(Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO )
Serikali
katika mwaka wa fedha 2015/2016 ilitenga Shillingi million 300 kwa
ajili matengenezo na ujenzi wa Barabara ya Kitosi- Wampembe katika
Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) ili
kufanya Barabara hiyo iweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.
Akijibu swali la Mhe.Desdelius John Mipata Mbunge wa Nkasi Kusini
(CCM) liliouliza ni lini Serikali itaitikia kilio hiki cha wananchi
wanaopata shida kwa Barabara hizo kutopitika katika kipindi chote cha
mwaka,Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin
Ngonyani amesema Serikali kupitia Wizara yake imesikia kilio cha
wananchi wa Wilaya ya Nkasi na inaendelea kutoa fedha za matengenezo ya
Barabara ya Kitosi-wampembe.
“ Kwa mwaka wa fedha 2014/2015 Serikali ilitoa jumla ya Shillimgi
Millioni 500 ili kufanya matengenezo ya Barabara ya Kitosi-Wampembe ili
ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka” Alisema Mhe Ngonyani.
Aidha ,katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/2015 Serikali
ilitenga jumla ya Shillingi Millioni 45 na Shillingi Millioni 60
zimetengwa katika mwaka wa fedha 2015/2016 kwa ajili ya matengenezo ya
aina mbalimbali ya barabara ya Nkana-Kala kupitia Halmashauri ya Wilaya
ya Nkasi ili kuhakikisha inapitika kwa kipindi chote cha mwaka.
Ukarabati wa barabara ya
Kitosi-Wampembe yenye urefu wa kilomita 67 na Barabara ya Nkana –kala
yenye urefu wa kilometa 68 uko chini ya Mfuko wa Barabara ikisimamiwa na
Wakala wa Barabara (TANROADS) na Barabara zote hizi ziko
chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ambayo inawajibika kuwezesha
Barabara zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka.
0 comments:
Post a Comment