Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
WATU
watatu wamekufa maji siku ya mkesha wa sikukuu ya Krismasi baada ya
gari aina ya Noa walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia mtoni.
Gari hilo la abiria lilikuwa likisafiri kutokana kijiji cha Muze wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa likielekea katika kijiji cha Majimoto wilayani Mlele mkoani Katavi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, Kalolo Joseph Ntila alisema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 24 nyakati za saa 4:20 usiku ambapo gari hilo likiwa na abiria saba lilipoacha njia na kutumbukia katika mto huo.
Alisema kuwa baada ya gari hilo kutumbukia kwenye mto Kilambo ambapo baadhi ya abiria walifanya jitihada za kujiokoa ambapo walifanikiwa kutoka huku wanawake wawili na mtoto mdogo mmoja walishindwa kutoka ndani ya gari hilo na kufa maji wakiwa ndani ya gari hilo.
Ntila ambaye ni Diwani wa Kata ya Muze, alisema kuwa baada ya abiria hao kutoka walijitahidi kutoa msaada kwa watu waliokuwa wamebaki ndani ya gari hilo lakini hawakufanikiwa kutokana na maji mengi na walipofanikiwa waliwatoa wakiwa wamefariki dunia.
Alisema kuwa watu hao bado hawajafahamika majina yao lakini miili ya marehemu hiyo ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha afya cha Muze kwaajili ya kusubiri kutambuliwa ili ndugu zao wakafanye maziko ya watu hao.
Aidha, Diwani huyo aliongeza kwamba eneo hilo ambalo ajali hiyo imetokea si nzuri hasa nyakati hizi za masika pindi mvua zinaponyesha kumekuwa na utelezi hali iliyosababisha gari hilo kuteleza na kutumbukia mtoni.
Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na kutaka madereva wanaofanya safari kupitia barabara hiyo kuwa waangalifu katika nyakati hizi za masika kwani kutokana uharibifu mkubwa wa barabara kwenye eneo hilo.
Mwisho.
MGANGA wa Jadi aliyefahamika kwa jina la Vitus Chomba(42) mkazi wa Sumbawanga mjini mkoani Rukwa anashikiliwa na polisi wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi baada ya kukutwa na nyara za serikali kinyume cha sheria.
Habari za uhakika kutoka eneo la tukio zinaeleza kwamba mganga huyo alikamatwa Desemba 27 nyakati za saa 1:00 za jioni, baada ya wakazi wa eneo alilokuwa akiishi kumtilia shaka kutokana na kukutana na watu kwa siri wakati yeye ni mgeni katika eneo hilo.
Akizungumzia tukio hilo afisa mtendaji wa kata ya Nsekwa wilayani Mlele mkoani Katavi Amos Ngozi alisema alipokea taarifa kutoka kwa wakazi wa kata hiyo wakieleza kuwa kuna mtu ambaye amekuwa akikutana kwa siri kubwa na baadhi ya wakazi wa kata hiyo hali iliyosababisha hofu kwa baadhi ya wananchi.
Alisema baada ya taarifa hizo alitoa taarifa polisi ambapo kwa kushirikiana na polsi hao walivamia katika nyumba anayoishi mganga huyo na kuanza kuifanyia upekuzi na katika beji lake la nguo walikuta kuna Ngozi ya simba, maini ya Swala pamoja na ngozi ya paka pori.
Mtendaji huyo wa kata alisema kuwa vitu vingine walivyokutwa navyo ni nyama ya Sungura, kwato za pundamilia pamoja na mkia wa nyati ambapo vyote thamani yake bado haijafahamika, vinavyodaiwa kutumia kwa ajili ya shughuli zake za uganga wa jadi na hutumia kwaajili ya kutibu ama kuroga kutokana na huduma anayohitaji mteja wake.
Alisema mganga huyo alifika katika kijiji cha Inyonga wilayani humo kwalengo la kufuata wateja wake ambao walikuwa wamemuita awatibu na kuwafanyia zindiko pia kutafuta vitu ambavyo atavitumia katika kutengeneza dawa ambazo anatumia kutibia wateja wake.
Hata hivyo, mtendaji Ngozi alisema mganga huyo alichukuliwa na polisi na kushikiliwa katika kituo cha polisi kutokana na kukutwa akiwa na nyara za serikali, kosa la kufanya tiba za jadi wakati hana kibali cha kufanya kazi hiyo.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi mkoa huo, Dhahiri Kidavashari alikiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na bado anahojiwa na polisi ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa ikiwa pamoja na kufikishwa mahakamani.

0 comments:
Post a Comment