Home » » NDUGU WAWILI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KILA MMOJA KWA KOSA LA KU

NDUGU WAWILI WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KILA MMOJA KWA KOSA LA KU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Watu wawili  Godfrey Kayumbi (30)   na  Luis Kayumbi(20) wakazi wa Kijiji cha Isenga  Tarafa  ya Mtowisa Mkoa wa Rukwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja baada ya kupatikana na kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha
Hukumu  hiyo ilitolewa hapo jana na Hakimu   Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa
Mwendesha  mashitaka  mwanasheria wa Serikali  K ulwa  Kusekwa  awali alidai kuwa watuhumiwa  hao   walitenda kosa hilo   Machi  20  mwaka huu majira ya samoja usiku  huko katika  maeneo    ya msitu  wa Mishamo Wilaya ya Mpanda
Siku hiyo ya tukio watuhumiwa  wanadaiwa walipora  pikipiki  Issa Moshi  yenye namba za usajiri  MC 644  AAV  aina ya Kinlaini  mali ya askari polisi wa kituo cha polisi cha Mishamo WP Happy  baada ya kumteka kwa kutumia silaha aina ya panga
Katika  kesi hiyo watuhumiwa  walikana kuhusika na tukio hilo kwa kile walichodai kuwa  hawakutenda kosa hilo bali wamesingiziwa
Mshitakiwa  wa kwanza katika kesi hiyo   Godfey  aliiomba Mahakama imwachie huru kwani yeye akutenda kosa hilo bali zilikuwa ni njama za mkuu wa kituo cha Polisi  cha Mishamo  ambae anatembea na mke wake  hivyo ameamua kumsingizia ili yeye  akafungwe jela ili  abaki amwowe mke wake
Mshitakiwa wa pili  aliiomba  Mahakama imwachie huru kwa kuwa   anaumri mdogo wa miaka  kumi na saba na wala  hakutenda kosa hilo  ombi hilo lilipingwa vikali na mwanasheria wa Serikali  ambae aliiomba  Mahakama  itowe idhini ya  mshitakiwa huyo kwenda kupimwa umri wake na Daktari
Hakimu Chiganga alikubaliana na ombi la Mwanasheria wa  Serikali  la kumpeleka mshitakiwa wa pili kwa  daktari ili kuweza kutambua umri halali wa mshitakiwa
Ushahidi  uliotolewa na Daktari  Mahakamani hapo ulionyesha kuwa mtuhumiwa  huyo  anaumri wa kati ya miaka 19 na miaka 20
Mahakama baada ya kusikiliza  pande mbili za mashitaka na utetezi ambapo upande wa mashitaka ulikuwa  na mashahidi 11 na washitakiwa hawakuwa na shahidi yoyote  Hakimu  Chiganga  aliieleza  Mahakama kuwa baada ya  kusikiliza mwenendo mzima wa kesi hiyo watuhumiwa wamepatikana na hatia ya  kosa la kifungu cha  sheria  287A  cha sheria ya  kanuni  ya adhabu  sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002
Hivyo  Hakimu Chiganga aliiambia  Mahakama kuwa  washitakiwa kutokana  na kutenda kosa hilo Mahakama imewahukumu kifungo cha kutumikia jela kila mmoja kifungo cha miaka 30 jela kuanzia jana

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa