Home » » WAONYWA KUHUSU KUWAPOKEA NA KUWAHFADHI WAHAMIAJI HARAMU.‏

WAONYWA KUHUSU KUWAPOKEA NA KUWAHFADHI WAHAMIAJI HARAMU.‏

Na Walter Mguluchuma.
Sumbawanga.
 
IDARA ya uhamiaji mkoa wa Rukwa, imewatahadharisha baadhi ya wananchi
kuacha kuwapokea na kuwawahifadhi wahamiaji haramu ambao wameanza kuingia
tena nchini kwa njia za panya baada ya kurejeshwa makwao wakati wa
operesheni ya kimbunga iliyofanyika mwaka jana.
 
Ofisa uhamiaji mkoa Seleman Kameya alisema hayo jana wakati akizungumza na
mwandishi wa habari hizi ofisini kwake aliyetaka kujua namna idara ya
uhamiaji ilivyojipanga kukabiliana na changamoto ya wahamiaji haramu
waliorejeshwa makwao kuanza kurudi tena nchini bila kufuata utaratibu.
 
Alisema kuwa operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu imekwisha kwa maana
ya muda lakini bado inaendelea hivyo basi ni vema wananchi wakatoa
ushiarikiano kwa idara hiyo na kwa viongozi wa vijiji na kata pindi
wanapobaini kuna wageni wameingia nchini bila kufuata utaratibu na si
kuwahifadhi kwani wakinaswa wote watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa
pamoja na kufikishwa mahakamani.
 
"Hatuna taarifa za wahamiaji haramu waliorejeshwa makwao kwamba wameanza
kurudi tena nchini kwa kupitia njia zisizo sahihi.....lakini nachoweza
kusema ni kwamba kwakushirikiana na viongozi wa kata na vijiji tumejipanga
vizuri kudhibiti wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume cha sheria na
tunaomba wananchi nao watusaidie kutoa taarifa" alisema Ofisa huyo.
 
Kameya aliongeza kwamba wahamiaji wengi haramu wamekuwa wakikimbilia nchini
hususani mwambao wa Ziwa Tanganyika kutokana na nchi zao kutokea machafuko
ya mara kwa mara ambapo wakiwa nchini upendelea kufanya shughuli za uvuvi
na biashara ya samaki.
 
Kwa mujibu wa Ofisa huyo, Operesheni hiyo iliweza kuondoa wahamiaji haramu
1900 ambao walirejeshwa kwa lazima na hiari katika nchi zao za Rwanda,
Burundi na Kongo DRC ambapo sehemu kubwa ilijikita kwenye maeneo ya vijiji
vya mwambao wa Ziwa Tanganyika.
 
Licha ya wahamiaji haramu kutoka nchini hizo za jirani, pia mkoa wa Rukwa
umekuwa ni njia ya wahamiaji wahamiaji haramu wenye asili ya kisomalia
ambao unaswa mara kadhaa wakisafiri kutoka nchini mwao wakielekea nchi za
Zambia na Malawi na Afrika Kusini.

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa