Ni kazi ngumu kumlea mtoto tangu anapozaliwa hadi kupevuka.
Hata hivyo, malezi bora kwa watoto wachanga ni
mkusanyiko wa mambo mengi yakiwemo lishe bora, malazi mavazi na tiba na
kinga ya maradhi.
Miongoni mwa mambo ya kuzingatia katila malezi ya
mtoto ni kumkinga na maradhi sambamba na kuuweka mwili wake katika
mazingira mazuri
Kama ilivyo muhimu kufanya mazoezi kwa watoto
wakubwa na watu wazima, watoto wachanga vile vile wanao umuhimu wa
kufanyishwa mazoezi.
Hivyo basi, mazoezi kwa mtoto mchanga ni miongoni
mwa mambo muhimu ya kuzingatia kwa wazazi au hata walezi wanaopewa
jukumu hilo.
Jambo la muhimu la kuzingatia kwa mzazi au mlezi
ni kuwa tayari kujifunza kila siku mbinu mpya zitakazosaidia kuboresha
na kufanikisha malezi stahiki ya mtoto mchanga hadi anapoondokana na
uchanga wake.
Vile vile, mzazi au mlezi hana budi kufahamu kuwa
kwa jinsi siku zinavyopita, na kwa kadri mtoto anavyokua, mambo
mbalimbali hujitokeza kwa mtoto hali inayopaswa kuendana na kasi ya
kujifunza kila siku ili kuelekea mafanikio.
Kwa kawaida ukiwa mama unapaswa kujifunza mambo
mengi kuhusu watoto kila kukicha na unapaswa pia kuhakikisha kile kitu
ulichojifunza unakifanyia kazi ili kumpa kichanga makuzi yanayostahili.
Tofauti inayopatikana hapa ni kuwa wakati makundi
hayo mengine hufanya mazoezi kwa kutumia nguvu zao, watoto wachanga
hupaswa kufanyishwa mazoezi na wazazi na walezi wao.
Mazoezi haya ya mtoto mchanga yanafanyika kwa
utaratibu wa massage ambapo kinachofanyika ni kumkanda au kumfanyia
masaji sehemu mbalimbali za mwili wake.
Watoto wanaposuguliwa taratibu tumboni hii huweza
kuwafanya wajisikie vizuri kwa vile huhisi kwamba angalau mzazi ama
mlezi anajitahidi katika kufanya kitu fulani kusaidia kumwondolea shida.
Jinsi ya kufanya
Ikumbukwe kuwa viungo vya mtoto mchanga ni laini, unapomfanyisha
mazoezi mtoto mchanga unapaswa kuepuka kutumia nguvu na badala yake
kuhakikisha unatulia na kufanya hivyo kwa uangalifu.
Masaji yenyewe iwe ni ile ya kumsugua taratibu
mgongoni, kumnyoosha viungo vya mwili wake hususani sehemu za miguu,
mikono pamoja na vidole.
Masaji hii inawekwa kufanywa kwa kutumia mafuta
laini ya mtoto, mafuta ya nazi yaliyotengenezwa na mama mwenyewe ni
mazuri kwa kuwa hayana kemikali.
Chanzo;Mwananchia
Chanzo;Mwananchia
0 comments:
Post a Comment