Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na uongozi wa
Wilaya ya Nkasi alipotembelea shamba la shule ya Msingi Matala ambalo
pia linatumika kama shamba darasa ukiwa ni mpango ulioanzishwa na
uongozi wa Mkoa wa Rukwa kusaidia elimu ya kilimo mashuleni na kusaidia
upatikani wa chakula kwa wanafunzi. Katika mpango huo kila shule Mkoani
Rukwa imetakiwa kuwa shamba ekari zisizopungua tano ambazo zitapatiwa
ruzuku ya pembejeo inayotolewa na Serikali na kusimamiwa na afisa ugani
wa eneo husika na kuwa shamba la mfano kwa wananchi katika Kilimo bora.
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Injinia Stella Manyanya kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika
ujenzi unaondelea wa mradi wa maji katika kijiji cha Matala Wilayani
humo jana.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiweka jiwe la msingi katika
ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Matala Wilayani Nkasi jana.
Mradi huo unaofadhiliwa na Serikali, mpaka kukamilika kwake
utatumia zaidi ya Tshilingi milioni 300. Jumla ya vijiji kumi (10)
katika wilaya ya Nkasi vinategemewa kupata maji ya uhakika kutokana na
miradi inayoendelea ambapo zaidi ya Tsh. Bilioni tisa zimeshatengwa
kukamilisha ujenzi wake. Changamoto zinazoikabili miradi hii ni
kuchelewa kwa fedha kutoka Wizara ya maji pamoja na uhaba wa mabomba na
viungio vyake kutoka viwandani.
Picha ya pamoja.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi jezi Kapteni wa
Timu ya Matala FC Filbert Ndiela kama moja ya kampeni zake Mkoani Rukwa
kuhamasisha michezo kwa vijana, ujasiriamali na kujituma katika shughuli
za maendeleo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta. Katika
hotuba yake Injinia Manyanya alitoa onyo kali kwa wananchi wenye tabia
ya kulima kwenye vyanzo vya maji na kuwaomba wananchi kujali afya zao
kwa kujitolea kupima VVU na kinamama wajawazito kujifungulia kwenye
vituo vya afya au zahanati.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya baada ya hotuba yake na kabla
ya kuondoka kwenye mkutano wa hadhara wananchi walimuomba awachezee
ngoma yao ya kabila la kifipa ambayo aliitendea haki vilivyo kama
anavyoonekana pichani kulia. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)





0 comments:
Post a Comment