Home » » MATUKIO YA MAUAJI YAPUNGUA MKOANI RUKWA

MATUKIO YA MAUAJI YAPUNGUA MKOANI RUKWA

Na Walter Mguluchuma-Sumbawanga
 MATUKIO ya mauaji  ya kikatili   yanayosababishwa  na  imani  za kishirikina  mkoani Rukwa  yamepungua hadi  kufikia  visa  30  mwaka jana  ukilinganisha  na matukio  37  yaliyoripotiwa  mwaka  2012.

Kwa mujibu  wa  Kamanda  wa Polisi  wa Mkoa  wa Rukwa , Jacob Mwaruanda kupungua  kwa mauaji  hayo  kunatokana  na  ushirikiano  wa  Jeshi la Polisi  na  wadau  wengine  wa  ulinzi  wakiwemo  waandishi  wa  habari na  wananchi .
Akifafanua  alisema kuwa   miongoni  mwa makosa  ya jinai  yaliyogusa  sana hisi  za  wakazi  wa  mkoani  hapa  na kwingineko  ni  pamoja na matukio  mawali  ambapo  watu  wenye uelemavu  wa ngozi ‘albino walivamiwa  na kukatwa  mkono  moja kila mmoja wao  katika matukio  tofauti .
“Pia matukio  ya  wanavijiji vinavvyozunguka  mashamba  ya Shrika la Ephata  wilayani Sumbawanga  kuvamia  mashamba hayo  na kuwapiga  walinzi , kuharibu  mazao  na  kuteketeza matrekta  kutokana na  mgogoro wa ardhi kati  yao “  alibainisha .
Kwa  mujibu  Mwaruanda  watuhumiwa  wa  matukio  hayo  walikamatwa  na mashauri  yao  yako katika  hatua  mbalimbali  za  kutolewa  maamuzi  mahakamani .
Kwa upande  wa  usalama  barabarani  alisema  kuwa  ajali za  barabarani  ziliendelea  kugharimu   maisha  ya  watu  ambapo  matukio   37 ya  ajali za barabarani  zilizotokea  mwaka  jana  zilisababisha  vifo 43  ambapo  mwaka  juzi  yaliripotiwa matukio  38  ya  ajali  za  barabarani  ambayo yaligharimu  maisha  ya  watu 57

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa