Home » » Pinda ataka ujenzi chuo kikuu

Pinda ataka ujenzi chuo kikuu

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, ameitaka mikoa ya ukanda wa Ziwa Tanganyika, ambayo ni Katavi, Rukwa na Kigoma, kushirikiana kujenga chuo kikuu walau kimoja, ili kuinua sekta ya elimu. Pinda alitoa kauli hiyo kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi, wakati wa mkesha wa kuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014.

Alisema mikoa hiyo inakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na chuo kikuu kinachotoa elimu ya juu, wakati mahitaji ya wanafunzi kusoma katika vyuo vikuu yanaongezeka siku hadi siku.


Alisema mpango wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo mkoani Katavi, ambao ulikuwa umesimama, sasa umeanza kufikia hatua nzuri kati ya Serikali, uongozi wa mkoa na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Alisema mpango huo wa ujenzi wa chuo hicho, ulikwama kutokana na mizengwe ya watu wachache.

Alisema kama chuo hicho kikianzishwa, kitakuwa mkombozi kwenye ukanda wa Ziwa Tanganyika, ambao kila mwaka umekuwa ukizalisha wanafunzi wengi.

Lakini wananchi wengi katika mkesho huo, walikuwa na kiu ya kusikia Pinda atazungumziaje hali ya kisiasa iliyotokea ndani ya kikao cha Bunge kilichomalizika hivi karibu na kusababisha mawaziri wanne kujiuzulu.

Pamoja na shauku hiyo, Pinda hakuwa tayari kueleza chochote juu ya sakata hilo.

Alisema Serikali imetenga Sh bilioni 11 kwa shughuli za maendeleo katika mji wa Mpanda, ambazo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa soko, stendi ya mabasi ya kisasa na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika maeneo ya mjini.

Pia Sh bilioni 4, zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kigoma–Mpanda kwa kiwango cha lami na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), imekubali kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya Mpanda-Tabora.

Chanzo;Mtanzania
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa