Mtoto wa mlalamikaji Abdulrahaman Zuber Bundallah ambaye alitoa maelezo kwa niaba ya baba yake George Donasy.
Na Hastin Liumba,Sumbawanga
“NILINUNUA nyumba kwa njia ya mnada uliokuwa
ukiendeshwa kupitia benki ya CRDB tawi la Sumbawanga lakini hadi leo hii benki
hiyo imeshindwa kunikabidhi nyumba hiyo licha ya kunikabidhi hati ya nyumba
baada ya kutoa malipo ya fedha taslimu kwa awamu.
Hayo ni maneno ya George Jibunge Donasy (69) mkazi
wa kijiji cha Namanyele wilaya Nkasi mkoa wa Rukwa wakati akiongea na mwandishi
wa makala hii kupitia mtoto wake Abdulrahaman Bndallah wilayani humo.
Donasy anasema alinunua nyumba iliyoko mtaa wa
Sumbawanga mwaka 2003 kwa njia ya mnada kwa thamani ya sh milioni 6,000,000
baada ya benki ya CRDB tawi la Sumbawanga.
Alifafanua kuwa baada ya mnada huo ulioendeshwa na
Dalali wa benki hiyo Salum Wastara alitakiwa na benki ya CRDB tawi la
Sumbawanga kulipa asilimia 25 kama masharti yanavyosema ambapo alilipa sh
milioni 1,500,000 hiyo ikiwa ni mwezi machi 3 mwaka 2003.
Aidha fedha nyingine ambazo alilipa kwa awamu ni sh
milioni 3,000,000 mwezi machi 13 mwaka 2003 na sh 700,000 mwezi juni 2003 na
mwezi agosti 4 mwaka 2003.
Alisema alitimiza masharti yote baada ya kumaliza
kulipa fedha kiasi cha sh milioni 6,000,000 na kukabidhiwa hati za nyumba namba
2086-DLR PLOT namba 114 Block KK.
Alisema licha ya kukabidhiwa hati za nyumba hiyo
bado benki ya CRDB imekuwa ikimzungusha kila mara alipotaka nyumba yake na
fedha sh milioni sita taslimu alishalipa.
Donacy alisema nyumba hiyo ilikuwa mali ya Luis
Msafiri na mke wake Cristoprina Msafiri ambao hadi leo hii wameendelea
kung`ang`ania ndani ya nyumba hiyo licha mimi kukabidhiwa hati ya nyumba hiyo
na benki ya CRDB tawi la Sumbawanga kuwa mmiliki halali baada ya kuinunua.
“Katika hali ya kushangaza benki ya CRDB wamefikia
hatua sasa wakanieleza kuwa nyumba niliyonunua iliuzwa kimakosa hivyo sistahili
kukabidhiwa hali ambayo naona haki yangu inataka kupokwa na kufanyiwa utapeli
wa waziwazi.” aliongeza.
Anafafanua kuwa Luis Msafiri na mke wake Cristoprina
Msafiri walifikia hatua ya makubaliano ya biashara na Aban Samson Ndenje na
alitaka kukopa benki kiasi cha sh milioni 40.
Alisema hajui kilichotokea kama makubaliano kati ya
Luis Msafiri na Aban Ndenje hadi wakakukubaliana kupeleka hati ya nyumba namba
2086-DLR Plot namba 114 Block KK kuomba mkopo wa sh milioni 40,000,000.
Donasy alisema kutokana na Aban Ndenje kudaiwa na
tawi hilo kutokana na mkopo wa sh milioni 15,000,000 ndipo hati hiyo
ilipozuiliwa na nyumba hiyo kuingia kwenye kuuzwa kwa njia ya mnada kufidia
deni hilo.
Anasema Aban Ndenje kipindi cha nyuma aliwahi kukopa
CRDB benki sh milioni milioni 15 lakini kutokana na kushindwa kurejesha mkopo
huo ndipo benki ya CRDB ilipokamata na kuuza nyumba yake iliyokuwa na hati
namba 1895-MBYLR na gari yake iliyokuwa na namba za kipindi hicho TZH 8713
kufidia mkopo wa sh milioni 15.
Donasy anafafamua kuwa baada ya kuona benki ya CRDB
tawi la Sumbawanga imemgeuka chini ya meneja wa Tawi Tom Ajwang Aduwa kwa madai
nyumba aliyonunua iliuzwa kimakosa ndipo alipoamua kukimbilia mahakamani
kushitaki hiyo ilikuwa mwaka 2009 kupitia wakili wake toka jijini Mbeya Justinian
Mushokora.
Alisema alifungua kesi ya madai mahakama ya wilaya
ya Sumbawanga dhidi ya Luis Msafiri,Cristoprina J Msafiri wenye nyumba,Aban
Samson Ndenje mkopaji wa sh milioni 15 za awali na sh milioni 40 alizotaka
kukopa na kuwashawishi Luis na Cristopina wakampa hati ya nyumba namba 2086-DLR
Plot namba 114 Block KK na benki ya CRDB tawi la Sumbawanga.
Aliongeza kesi hiyo yenye namba Civil Case 8/201
mahakama ya wilaya Sumbawanga alishinda hiyo mwaka 2009 na wadaiwa
hawakuridhika licha mahakama hiyo kuwataka kunikabidhi nyumba yangu lakini
walikaidi na kesi ilirejea tena mahakamani.
Alisema kesi hiyo ilirejea makahakama ya wilaya ya
Sumbawanga tena mwaka 2012 akashinda na danadana ziliendelea hadi kesi hiyo
ilirejea tena mahakamani mwaka 2013 na alishinda kwa mara ya tatu mfululizo.
“Licha ya mahakama kunipa ushindi kwa mara tatu
mfululizo bado benki ya CRDB tawi la Sumbawanga,bado sijapata nyumba yangu hadi
leo lakini nasikia kuna mipango ya kuiuza nyumba hiyo upya kwa tajiri mmoja
ambaye awali alishanitafuta kutaka nipokee kiasi cha sh milioni 20,000,000
niachane na madai hayo.”anaongeza.
Alisema suala hilo pia baada ya kumshirikisha mtoto
wake aliyeko mkoani Tabora Abdulrahaman Zuber Bundallah tajiri huyo namuhifadhi
jina alimpigia simu mwanangu wakakutana Sumbawanga na alimueleza anishawishi
mimi safari hii nikubali kupokea sh milioni 75,000,000 kati ya milioni
90,000,000 ninazodai kama gharama ya kuendeshea kesi mahakamani pia nilikataa.
Alisema anachotaka ni kukabidhiwa nyumba aliyonunua
na kiasi cha sh milioni 90,000,000 kama gharama za kesi aliyoendesha mahakama
ya wilaya Sumbawanga.
Anasema katika hai ya kusikitisha licha mahakama
kunipa ushindi na kuagiza nipewe haki yangu hadi sasa naangaishwa na haki yangu
naona inatakaka kupotea sijui nikimbilie wapi.
Alisema benki ya CRDB tawi la Sumbawanga baada ya
kufanyika kwa mnada na kuuzwa nyumba hiyo walimkabidhi hati ya nyumba hiyo
mwaka 2004 na kudai amenunua nyumba kihalali hivyo taratibu zitafanyika apewe
nyumba hiyo.
Alisema alisoma tangazo la mnada mnamo mwezi
februari 13,2003 kuwa kuna mnada wa kuuzwa vitu mbalimbali ikiwemo nyumba hiyo
kutokana na wakopaji walioshindwa kurejesha mkopo waliouchukua benki ya CRDB.
Alisema kutokana na mazingira hayo ya kitapeli bado
ameendesha kesi ya kudai haki yake lakini benki wanakaidi maagizo ya mahakama
alifungua madai ya gharama za kuendesha kesi hiyo ya sh milioni 90,000,000 kesi
ambayo alishinda kesi mara zote tatu kila ilipofikishwa mahakakani.
Kwa upande wake mtoto wa mnunuzi wa nyumba hiyo
George Jibunge Donasy, Abdulrahaman Zuber Bundallah alikiri baba yake kununua
nyumba na hadi sasa yeye ndiye analisimamia jambo hilo kwani baba yake umri
wake ni mkubwa na anahitaji kupata muda wa kupumzika.
Bundala pia alikiri kufuatwa na tajiri mmoja
aliyemtaja kwa jina moja la Said na kushawishiwa wakubali yeye na baba yake
kuchukua sh milioni 75,000,000 ili waachanane na madai y ash milioni 90,000,000
na warejeshe hati ya nyumba benki lakini alimkatalia.
Kwa upande wao Luis Msafiri na mke wake Cristoprina
Msafiri walikiri kuwahi kufanyika kwa mnada na nyumba yao ikauzwa lakini
imeuzwa kimakosa na wanachotaka sasa ni kufungua kesi ili arejeshewe hati ya
nyumba yake.
Naye Aban Ndenje alipotakiwa kuzungumzia suala la
kuingia kwenye mgogoro wa nyumba hiyo ilipigwa mnada na kufilisiwa kwa baadhi
ya mali zake hakutaka kuongea chochote na kudai hana majibu.
Kwa upande wake meneja wa CRDB tawi la Sumbawanga
Tom Ajwang Aduwa alikiri kutambua suala hilo lakini akasema kwa sasa hawezi
kulizungumzia suala hilo atafutwe siku nyingine kwa muda ule ana majukumu
mengine ya kiofisi.
Alisema maelezo mengine hayafahamu vyema kwani
wakati suala hilo linaanza hakuwepo kituo cha kazi Sumbawanga kama meneja.
0 comments:
Post a Comment