Sumbawanga. Wananchi waliotaka kujichukulia
sheria mikononi, nusura walichome moto gari la wagonjwa lilitolewa
msaada Kituo cha Afya Mtowisa wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa kutokana
na madai ya kuchangia kifo cha mwalimu mmoja aliyekosa msaada wa haraka
wakati wa kujifungua.
Wananchi hao wanadaiwa kulishambulia gari hilo kwa mawe na kuvunja moja ya kioo.
Gari hilo linadaiwa kuchelewa kuja kumchukua
Mwalimu Leah Mgaya wa Shule ya Msingi Mtowisa ‘A’, ambaye alifariki
baada ya kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua.
Habari kutoka sehemu ya tukio zilizothibitishwa na
Ofisa Tarafa ya Mtowisa, Peter Masindi zinaeleza kuwa, awali mwalimu
huyo alipelekwa katika kituo hicho cha afya juzi saa 3 asubuhi akiwa
katika hali uchungu wa kujifungua, lakini baadaye ilionekana anahitaji
kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa.
Masindi alisema kutokana na hali hiyo ililazimu
kupiga simu Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya saa 6 mchana ili kuomba
msaada wa gari, lakini gari hiyo ilichelewa kufika kutokana na kudaiwa
ilisafiri kwenda wilayani Nkasi, na hata iliporejea jioni ilikwama
njiani kutokana na hali ya mvua.
Mmoja ya wananchi waliozungumza na gazeti hili,
Mwaipungu alisema kifo cha mwalimu huyo kiliwakera wananchi wa eneo
hilo, ambapo walikusanyika kwenye makundi na kuanza kujadiliana.
Wananchi hao walidai kuwa gari hilo la wagonjwa halina msaada kwani muda mwingi haliko kituoni hapo hivyo kutaka kulichoma moto.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment