Home »
» Wafanyabiashara wahimizwa kununua mashine za TRA
Wafanyabiashara wahimizwa kununua mashine za TRA
|
|
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Rukwa imehimiza
ununuzi wa mashine za kutolea stakabadhi ya manunuzi kwa
wafanyabiashara wa kati kwa kuwa zina manufaa kwa mfanyabiashara, pia
zitachangia kuongeza makusanyo ya kodi.
Meneja wa TRA Rukwa, Philipo Kimune, alisema hayo jana wakati
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu uzinduzi wa
Wiki ya Mlipa Kodi itakayofikia kilele Novemba 8, mwaka huu.
Meneja Kimune alisema lengo ni kuhakikisha wafanyabiashara 2,213
waliopo Rukwa wananunua mashine hizo ambapo hadi sasa tayari
wafanyabiashara 100 wamenunua.
Meneja huyo alikiri kwamba pamoja na gharama kubwa ya kununua mashine
inayouzwa sh 800,000 lakini serikali kupitia mamlaka hiyo imeweka
utaratibu mzuri wa kurudisha fedha hizo kwa wafanyabiashara mara tu
baada ya kutengeneza hesabu za mwaka.
Kwa mujibu wa Kimune, Wiki ya Mlipa Kodi mwaka huu inaadhimishwa kwa
kufanyika shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa msaada
hospitalini, kituo cha watoto yatima cha Bethania na Gereza la Rukwa.
CHANZO;TANZANIA DAIMA
|
|
0 comments:
Post a Comment