UONGOZI wa Klabu ya waandishi wa
habari mkoani Rukwa (RKPC), umewazuia wanachama wake ambao ni waandishi wa
habari kuacha mara moja kuandika na kutangaza taarifa zozote zinazomhusu Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya kwa madai ya kutoa kauli za kuwadhalilisha
waandishi wa habari wa mkoa huo
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
Klabu hiyo ya waandishi wa habari mkoani humo , Peti Siyame alisema
jana kuwa uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha dharura cha
Kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo.
Ambapo kikao hicho pamoja na mambo mengine kilipokea taarifa ya kile kilichojili kwenye kikao cha kamati ya ushauri wa mkoa wa Rukwa (Rcc) ambapo kiongozi huyo wa Serikali inadawa kutoa lugha zisizopendeza kwa waandishi hao.
Ambapo kikao hicho pamoja na mambo mengine kilipokea taarifa ya kile kilichojili kwenye kikao cha kamati ya ushauri wa mkoa wa Rukwa (Rcc) ambapo kiongozi huyo wa Serikali inadawa kutoa lugha zisizopendeza kwa waandishi hao.
" Maamuzi hayo
yalifikiwa Septemba 28 mwaka huu katika kikoa cha
dharura cha Kamati ya Utendaji ya Rukwa Press Klabu baada ya
kujadili kwa kina kauli ya maudhi, kejeli, dharau, udhalilishaji na unyanyasaji
dhidi ya waandishi mbele ya wajumbe wa Rcc zaidi ya 70 kwenye kikao
kilichofanyika mjini Laela wilayani Sumbawanga" alisema Siyame.
Siyame pasipo kufafanua kuali
hiyo zilizowakera waandishi hao lakini alidai kuwa rungu hilo pia limemwangukia
katibu tawala wa mkoa wa Rukwa Salum Chima ambaye amekuwa hana mahusiano mazuri
na waandishi kwa muda mrefu sasa.
Amesisitiza kwa mahusiano hayo
yatarejea tu baada ya mkuu huyo wa mkoa na msaidizi wake watakawaomba radhi
waandishi kwenye kikao kijacho cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) kwani ndio
alikozungumza lugha zisizo sahihi dhidi ya wanahabari hao.
"Sisi tuliamini kwamba mkuu
wa mkoa hakutumia busara kabisa.....alipaswa atuite pembeni kama kuna tatizo na
kutueleza sio kuzungumza kwenye hadhara ya watu....wengine ni wadau wetu
wakubwa tunaheshimiana wanajua mchango wetu kwenye maendeleo ya mkoa huu, ndio
maana alivyoongea wengine waliguna na kucheka.
Alienda mbali zaidi na kueleza
kuwa kufanya kazi za kutangaza mkoa sio kumwandika yeye binafsi, sasa yeye
anataka aandikwe yeye tu ndio ionekane unatangaza mkoa....kamwe hatuwezi
kufanya hivyo, tutafanya kazi kwa maslahi ya umma sio yeye" aliongeza
Mwenyekiti huyo
Manyanya tayari ameanza kuonja
chungu ya waandishi kutofanya nae kazi baada ya juzi waandishi kuondoka wakati
akipanda jukwaani katika hafla fupi ya kukabidhi nyumba 20 zilizojengwa na
Taasisi ya Mkapa Foundation kwa watumishi wa afya iliyofanyika kwenye kijiji
cha Chipu.
Pia wanahabari hao juzi walikataa
mwaliko wake wakati makamu wa kwanza Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Maalim Seif Shariif Hamad, alipokuwa mkoani Rukwa kwa ajili ya kufunga Sherehe
za kiislamu za Hija ndogo (Jitimai).
Mgogoro wa waandishi hao na
viongozi wa Serikali ni wa pili baada ya mwaka 2007 walitangaza kuvunja
uhusiano wa kikazi na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa Germanus
Mpongoliana baada ya kuwazuia kufanya kazi wakati wa ujio wa Mkuu wa jeshi la
polisi Nchini Said Mwema.
Busara za umoja wa Klabu za waandishi wa habari nchini
(UTPC), Baraza la Habari na Mwema mwenyewe ndio zilizorudisha mahusiano kati ya
waandishi na Kamanda huyo.
0 comments:
Post a Comment