Serikali
mkoani Rukwa imesema upo umuhimu wa kuanza kutekeleza mpango wa kuwachukulia
hatua za kisheria na za kinidhamu maafisa afya wa mkoa huo watakaobainika
kuzembea katika kusimamia suala la usafi wa mazingira katika maeneo yao lengo
ikiwa ni kuzuia magonjwa ya mlipuko ya mara kwa mara.
Akizungumza na wadau wa afya katika kikao kilichowashirikisha pia
wakuu wa wilaya pamoja na viongozi wengine watendaji wa mkoa wa Rukwa,mkuu wa
mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa utaratibu huo utakwenda
pamoja na kuwafukuza kazi maafisa afya watakaobainika kushindwa kutimiza
majikumu yao ipasavyo.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa wa Rukwa
amelazimika kutoa msimamo huo mkali kufuatia kusuasua kwa kampeni ya usafi wa
mazingira ijulikanayo kwa jina la sumbawanga ngara iliyozinduliwa mapema mwaka
jana na makamu wa rais iliyolenga kuwa na mikakati endelevu ya kusimamia usafi
wa mazingira.
0 comments:
Post a Comment