Na Walter MguluchumaRukwaWATU wasiofahamika wamevamia nyumba ya mwanamke mwenye ulemavu waNgozi Albino Maria Chambanenje (39) mkazi wa kijiji cha Kavifutikilichopo katika wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa na kishakumkatakata kwa mapanga na kutoweka na mkono wake wa kushoto.Hata hivyo tukio hilo la kusikitisha lilitokea wakati mume wa mlemavuhuyo mwenye wake wawili akiwa ameenda kulala nyumba jirani ambayoni ya mke mkubwaAkizungumza mara baada ya kumfikisha mlemavu huyo wa ngozi katikahospitali ya mkoa wa Rukwa kwa ajili ya matibabu mume wa mlemavu huyowa ngozi aitwae Gabriel Yohana ,amesema kuwa tukio hilo la mkewekukakwa kwatwa kwa mapanga na kisha watu hao kuondoka na kipandecha mkono wa kushoto wa mkewe, lilitokea majira ya saa nane usikumara baada ya watu hao kuvamia nyumba ya mama huyo huku wakiwawamefunga milango ya nyumba za majirani kwa kamba kwa lengo lakuwazuia majirani hao wasitoe msaada wakati wa tukio hilo.Bw Yohana amesema kuwa usiku wa kuamikia leo majira ya saa 8 usikualifuatwa na mtoto wa kaka yake ambaye alidai kuwa nyumbani kwao,nyumba ambao analala mama huyo mlemavu wa ngozi kuwa kuna dalili zawatu kukata nyumba kwa kwa panga na kuwa amesikia sauti za watoto wamlemavu huyo wa ngozi zililia kwa kuomba msaada.Aliema kuwa hata hivyo mara baada ya kufika nyumbani hapawalimkutamkewe akiwa tayari amekatwa mkuno wake wa kushoto pamoja na kujeruhiwasehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani pamoja na mkono wakewa kulia na ndipo alipoanza kupiga kelele za kuomba msaada nakugundua ya kuwa nyumba za majirani zimefungwa kwa kamba nje kwalengo la kuzuia majirani hao kutoa msaada kwa mama huyo.Kwa upande wake daktari wa zamu wa hospitali ya mkoa wa Rukwa kitengocha tiba za nje Dkt rajabu Lugwashi amekiri kumpokea mama huyomwenye ulemavu wa ngozi na kusema kuwa mpaka sasa anaendelea kupatiwamatibabu ikiwemo kuongezewa damu kutokana na kuvuja damu kwa wingimara baada ya tukio hilo.Amesema kuwa mama huyo aliyekatwa mkono wa kutosho eneo la kiwikoanaendea kupatiwa matibabu na kuongeza kuwa majeraha yaliyopo katikamaeneo mbalimbali ya kichwa chake aliweza kufikishwa katika kituo chaafya cha Laela kilichopo umbali kidogo toka katika eneo la tukio nakushonywa.Kwa upande wao watendaji wa jeshi la polisi mkoa wa Rukwa walipohojiwajuu ya tukio hilo walishindwakutoa ushirikiano kwa madai ya kuwatukio hilo kuna mtu maalum anayelishugurikia.
Home »
» HATARI: ALBINO AVAMIWA NA KUKATWAKATWA NA WATU WASIOJLIKANA KISHA KUONDOKA NA MKONO WAKE WA KUSHOTO
HATARI: ALBINO AVAMIWA NA KUKATWAKATWA NA WATU WASIOJLIKANA KISHA KUONDOKA NA MKONO WAKE WA KUSHOTO
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
0 comments:
Post a Comment