Home » » WILAYA MPYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA MSHINDI WA KWANZA WA SHUGHULI ZA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2012 KANDA YA IV ILIYOSHINDANISHA MIKOA MITANO

WILAYA MPYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA MSHINDI WA KWANZA WA SHUGHULI ZA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2012 KANDA YA IV ILIYOSHINDANISHA MIKOA MITANO


Mkuu wa Wilaya mpya ya Kalambo Moshi Chang'a ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kwenye shughuli za kuzima Mwenge wa Uhuru Mkoani Shinyanga akionyesha Kikombe na Cheti alichokabidhiwa na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama zawadi ya ushindi kwa Wilaya yake baada ya kushika nafasi ya kwanza katika shughuli za mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 katika kanda ya nne iliyohusisha Mikoa mitano ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya zake alipowasili jana Mkoani Rukwa aikitokea Shinyanga. 
Hati kuithibitisha Wilaya ya Kalambo kutoka Mkoa wa Rukwa kuwa mshindi wa kwanza wa shughuli za mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 katika kanda ya nne iliyohusisha Mikoa mitano ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya zake.
Wawakilishi wa Mkoa wa Rukwa waliokwenda kushiriki kuzima mwenge wa uhuru Mkoani Shinyanga na kurudi na kikombe cha ushindi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a, mratibu wa Mwenge Kimkoa Abubakar Serungwe na Katibu wa Mkuu wa Mkoan Frank Mateny wakipewa mapokezi na uongozi na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.(Picha na Hamza Temba-rukwareview.blogspot.com-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa