Home » » WANANCHI WATEKETEAZA MATREKTA KATIKA SHAMBA LINALOMILIKIWA NA KANISA LA EFATHA HUKO SUMBAWANGA

WANANCHI WATEKETEAZA MATREKTA KATIKA SHAMBA LINALOMILIKIWA NA KANISA LA EFATHA HUKO SUMBAWANGA


Matrekta hayo yakiwa yameteketea kabisa kwa kuchomwa moto katika shamba hilo inalomilikiwa na kanisa la Efatha mkoani Rukwa.
Matrekta hayo yakiwa yameteketea kabisa kwa kuchomwa moto katika shamba hilo inalomilikiwa na kanisa la Efatha mkoani Rukwa.
Moja
ya makambi yaliyoteketea kwa kuunguzwa na moto wakati wananchi hao
walipovamia mashamba hayo na kuchoma moto zana za kilimo katika shamba
hilo.

(PICHA,  HABARI  NA JOSHUA MWAKABUNGU WA FULLSHANGWE SUMBAWANGA)

……………………………………………….

Shamba la Malonje linalomilikiwa na Kanisa la Efatha limepata hasara kubwa baada ya wananchi wa kijiji cha Sikaungu wilayani Sumbawanga vijijini mkoani Rukwa, kujichukulia sheria mkononi na kuvamia moja ya kambi ya Shamba hilo iitwayo Sikaungu na kuyateketeza kabisa matrekta mawili makubwa aina ya New Holland na kubomoa baadhi ya nyumba kwenye kambi hiyo.






Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa la Efatha mkoani Rukwa akiongelea kuhusu suala hilo alisema hasara liyopatikana ni zaidi ya shilingi milioni 228 na kwamba tukio hilo lilitokea mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh. Ignas Malocha
kuhutubia mkutano wa hadahara kijijini hapo na kuwahamasisha wananchi
watumie nguvu ya umma  kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na
mwekezaji huyo.


Kamnda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda akithibitisha kuhusu sakata hilo alisema tayari wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kufanya uharibifu huo mkubwa na kwamba wanatarajiwa kufikishwa wakati wowote mahakamani
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa