Home » » UAMSHO WASHAURIWA KUJIENDELEZA KIELIMU

UAMSHO WASHAURIWA KUJIENDELEZA KIELIMU

Mwandishi wetu, Rukwa Yetu

KIKUNDI cha wanawake wajasiriamali  cha Uamsho kilichopo katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, kinachojumuisha wanawake wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na wale Taasisi binafsi kimeshauriwa kufanya biashara zao kwa wenyewe kujiunga na elimu za vyuo  mbalimbali kwa lengo la kuongeza ufanisi wao  katika biashara.

Ushauri huo umetolewa  na Mkurugenzi  wa Chuo Kikuu Huria Tawi la Rukwa , Dk Elna Lyamuya mara baada ya Mkuu wa Mkoa  huo , Mhandisi Stella Manyanya kuitisha kikao cha pamoja watendaji wake wa kike  kilicholenga kuunda kikundi hicho ,chenye lengo la kubadilishana uzoefu wa kibiashara zinazofanywa wa wanawake hao mara baada ya shughli zao za kiofisi kukakilika  kwa lengo la wao kujiongezea kipato

Dk Lyamuya amesema ili wanawake hao waweze kujikomboa na kufanya biashara zao kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia ni lazima wajikite katika elimu itakayowasaidia katika kunufaika na biashara zao wanazozifanya ,zikiwemo zile za usindikaji wa vyakula,uuzaji wa nafaka na ufugaji.

Mkuu wa Mkoa huo Rukwa, Mhandisi  Manyanya amesema lengo la kuunda umoja huo  ni pamoja  na  kuelimisha wanawake wengine kuondokana  na dhana tegemezi  ikiwa ni pamoja na kuona wanawake wanahamasika  kusoma ili kuweza kuendana na kasi ya  mabadiliko katika soko  huria la kibiashara..
Blogzamikoa

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa