Home » » MWAMUZI AJITOSA UONGOZI SOKA RUKWA

MWAMUZI AJITOSA UONGOZI SOKA RUKWA

Na Rahel Pallangyo
MWAMUZI wa soka ambaye pia ni Katibu wa Chama cha Waamuzi (FRAT) Mkoa wa Rukwa, Anthony Kayombo, amejitosa kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa chama cha soka mkoa wa Rukwa.

Anthony Kayombo, ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya Magereza Rukwa, amesema ameamua kugombea nafasi hiyo muhimu na ya utendaji, baada ya kuona soka katika mkoa wa Rukwa kuwa linadidimia kila kukicha.

Alisema anataka kurudisha mshikamano uliokuwepo zamani, kwani umepotea kwa sasa baada ya uongozi uliokuwepo kuacha kushughulikia masuala yanayohusu soka kwa ujumla na kuhangaikia shughuli za binafsi zaidi.

"Unajua Rukwa ulikuwa ni mkoa ambao umewahi kutoa timu ambazo zilileta sifa, lakini zilikufa na hakuna kiongozi ambaye alikuja na mikakati ya kuzifufua, hivyo

mimi kwa sababu nimewahi kucheza mpira na ni mwamuzi, nina uchungu wa kufufua soka kwa kushirikiana na wadau wengine na viongozi wenzangu watakaochaguliwa," alisema Kayombo.

Wagombea wengine kwenye nafasi ya Mwenyekiti ni Nazalius Kilungege, Blas Kiondo na Norbet Machesha.

Wengine wanaogombea nafasi ya katibu ni Field Kasitu na Gregory Seko, wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF ni Summy Kisika na John Maholani na mjumbe wa kuwakilisha vilabu ni Ayoub.
Chanzo: Mtanzania

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa