Home » » SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WANAOLANGUA MAFUTA RUKWA

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WANAOLANGUA MAFUTA RUKWA



Mussa Mwangoka, Sumbawanga.

UONGOZI wa Serikali mkoani Rukwa, umesema kuwa hautasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa baadhi ya wamiliki wa vituo vya uuzaji wa Nishati ya mafuta ya vyombo vya moto watakaobainika kufanya biashara ya ulanguzi wa bidhaa hiyo.

Tishio dhidi ya walanguzi wa bidhaa hiyo linakuja kutokana na kuwepo kwa tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wa mafuta hayo kugoma kuuza mafuta mara tu mamlaka ya udhibiti wa nishati ya mafuta na maji (Ewura) inapotangaza kushuka kwa bei ya mafuta, hivyo kutoa mwanya kwa kufanyika biashara ya ulanguzi ambapo bie ya mafuta ya petroli uuzwa hadi Sh 10,000 kwa lita.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya alisema hayo jana ofisi kwake wakati akizungumza na mwaandishi wa habari hizi aliyetaka kujua mikakati ya Serikali katika kudhiti tatizo la baadhi ya wamiliki wa vituo vya mafuta kugoma kuuza bidhaa hiyo mara baada ya Ewura kutangaza kushuka kwa bei, tatizo ambalo linajitokeza mara kwa mara.

Alisema ipo tabia ya baadhi ya wenye vituo vya mafuta mjini Sumbawanga kugoma kuuza bidhaa hiyo mara bei inaporemka na kutangazwa na mamlaka husika hivyo baadhi ya vijana kuuza kwa bei ya kulangua kitu ambacho ni kinyume na sheria.

"Sasa itabidi tutumie sheria ya kudhibiti ulanguzi ili kuwabana baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu ambao bei inaposhuka ugoma kutoa huduma hiyo katika vituo vyao na kuwatumia vijana kufanya biashara ya ulanguzi ambayo inawaumiza watumiaji wa huduma hiyo" alisema Manyanya.

Aliongeza kuwa licha ya kuwakamata watu wanaofanya biashara ya ulanguzi huo, pia kuna mazungumzo yanaendelea baina ya ofisi yake na Ewura kuona hatua  zaidi ambazo zitachukuliwa dhidi ya wafanyabiashara hao.

Kadhia ya inayosababishwa na kuadimika kwa nishati ya mafuta hususani petroli mara kwa mara imekuwa sugu, ambapo inasababisha kuuzwa mitaani na bei kuwa juu zaidi hali ambayo ilisababisha baadhi ya wananchi kuitupia lawama mamlaka husika kuwa imeshindwa kuwadhibiti wafanyabiashara wa mafuta mkoani Rukwa.

Blogzamikoa


Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa