Home » » BODABODA 200 WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI RUKWA

BODABODA 200 WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI RUKWA

Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya akizungumza na vijana ambao ni madereva wa pikipiki maarufu kwa jina la boda boda juzi kwenye moja kituo cha bodaboda hizo alipowatembelea ili kujionea kama hali usafiri huo umerejea kama kawaida baada ya kutokea ukosefu nishati ya mafuta. Picha na Mussa Mwangoka.
--------------------------------
Mussa Mwangoka, Sumbawanga.

POLISI mkoani Rukwa, kupitia kitengo cha usalama barabarani kimesaidia vijana wapatao 200 ambao ni maderereva bodaboda kupata elimu ya sheria za usalama barabarani.

Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Rukwa, mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP), Boniface Mbao alisema hayo jana wakati wa kikao baina ya madereva bodaboda na mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa mkoa huo (RDC).

Mrakibu huyo msaidizi wa Polisi, alisema jana kuwa kitengo cha usalama barabara kwa kushirikiana na chuo cha ufundi stadi cha Furaha Center kilichopo mjini Sumbawanga waliingia makubaliano ya kuhakikisha vijana hao wanapata elimu ya usalama barabara itakayowasaidia kuweza kumudu kuendesha vyombo vyao vya moto kwa kuzingiatia sheria.

"tuliona njia ya kuwasaidia si kuwakata kata hivyo tulizungumza na wenzetu wa chuo cha Furaha Center na tukakubaliana kuhusu vijana wa bodaboda kupata punguzo la ada ili waweze kujifunza sheria za barabarani, ambapo katika kipindi cha miezi 3 ada ilikuwa Sh 90,000 sasa imepunguzwa kwa vijana hao hadi kufika Sh 40,000 kwa miezi yote mitatu" alisema.

ASP Mbao mafunzo hayo ambayo yamewafikia vijana  200 kati ya madereva zaidi ya 300  yatawasaidia kupunguza ajali za boda boda ambazo ndizo idadi yake ni kubwa ukilinganisha na vyombo vingine vya moto, ambapo mara baada ya kumaliza mafunzo hayo, watakabidhiwa leseni.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya, alionya tabia ya baadhi ya waendesha bodaboda kuruhusu pikipiki zao kutumika kwa matukio ya uhalifu na kuwataka waache mara moja kwani watakaobainika sheria itachukua mkondo wake.

Pia Manyanya alisema kuwa wanapaswa kuheshimu kazi yao kwa kuwa wakiifanya vizuri ina kipato kikubwa kuliko kazi nyingine za maofisini ndio maana baadhi ya watu wenye elimu ya kuwawezesha kupata ajira Serikali na kwenye sekta binafsi wakiwamo walimu na wahasibu wamejikita kufanya biashara hiyo.
Blogzamikoa

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa