Home » » WIZARA YAKILIMO YATAKIWA KUZALISHA MBEGU ZITAKAZOHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI

WIZARA YAKILIMO YATAKIWA KUZALISHA MBEGU ZITAKAZOHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI

Mussa Mwangoka, Mpanda-Rukwa Yetu

IMEELEZWA kuwa ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchini zinazoanza kujitokeza nchini wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imeshauri kuboresha utafiti wa mbegu bora zenye uwezo wa kuzalisha mazao ya chakula kwa muda mfupi zaidi.

Katibu Mtendaji wa Muungano wa Asasi zisizo za Kiserikali mkoani Rukwa (Rango), Stanley Mshana alisema hayo jana wakati mdahalo wa kuelimisha wananchi kuhusu mabadiliko ya tabianchi uliofanyika katika kijiji cha Songambele, kata ya Nsimbo wilayani Mpanda na kufadhiliwa na shirika la Civil Society For Foundation.

 Alisema kuwa athari za mabadiliko ya tabianchi zimeanza kuathiri uzalishaji wa mazao ya chakula kwenye baadhi ya maeneo nchini hivyo hatua zinazotakiwa kuchukuliwa na serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa kilimo ni kuboresha tafiti ili kupata mbegu bora ambazo zitakuwa na uwezo wa kuzalisha mazao ya chakula kwa muda mfupi sana ukilinganisha na ilivyo sasa.

"utafiti ufanyike ili tupate mbegu bora zenye uwezo wa kuzalisha mazao kama mahindi katika kipindi cha kati ya mwezi mmoja hadi miwili hata ukame unapotokea ni rahisi kuendelea kupata mazao ya chakula ikibidi na biashara" alisema Mshana.

Aliongeza kuwa mabadiliko hayo hayaepukiki kwa sasa kutokana kuwepo kwa uharibifu mkubwa mazingira uliofanywa katika chini ulaya ambapo athari zake zinafika hadi afrika hivyo ni muhimu kuendelea kuwaelimisha wananchi kuepuka kuendelea na uharibifu wa mazingira kwa kukata miti na kuchomo moto misitu ili kuepuka hali kuja kuwa mbaya zaidi sasa.

Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho, Elizabeth Msafiri aliomba wapatie elimu ya namna ya kutengeneza majiko banifu na sanifu ambayo  yanatumia nishati kidogo ya mkaa hali itakayochangia kupunguza kasi ya ukataji miti na misitu ovyo.

Alisema kuwa taasisi nyingi zisizo za kiserikali zimekuwa zitoa elimu hiyo kwenye maeneo mengine hivyo sasa ni muhimu na  wao wakapata fursa ya kupata elimu hiyo kwani uzoefu unaonyesha kuwa majiko hayo yamekuwa wakisaidia sana kupunguza uharibifu wa mazingira.

Blogzamikoa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa