Home » » UJENZI WA BARABARA YA TUNDUMA-S’WANGA KUCHELEWA KUKAMILIKA

UJENZI WA BARABARA YA TUNDUMA-S’WANGA KUCHELEWA KUKAMILIKA

Mussa Mwangoka, Sumbawanga.

DALILI za kutokamilika kwa wakati ujenzi wa barabara ya Tunduma hadi Sumbawanga inayojengwa kwa kiwango cha lami zimeanza kuonekana baada ya baadhi ya kampuni za ukandarasi zinazojenga barabara hiyo kuomba kuongezea muda zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa iliyotolewa juzi katika kikao cha bodi ya barabara ya mkoa wa Rukwa, Meneja wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) mkoa huo, Mhandisi Florian Kabaka, ilisema kuwa ujenzi wa barabara hiyo unaofadhiliwa na fedha kutoka Serikali ya Marekani kupitia mfuko wa changamoto za Milenia (MCC) zipo shakani kukamalika kwa wakati.

Alisema kuwa kampuni ya Aarsleff - BAM International Joint Venture V.O.F tayari imeomba kuongezewa muda ili iweze kumaliza ujenzi wa kipande cha barabara ya Laela hadi Sumbawanga.

Kipande hicho cha barabara kina urefu wa kilometa 95.31 ambacho ujenzi wake ulipangwa kukamilika januari 31 mwaka mwakani lakini tayari wameomba kuongezewa muda zaidi hadi mei 31 mwaka 2013 ambapo hadi sasa maendeleo ya kazi ni asilimia 40 tu.

Mhandisi Kabaka, alisema kuhusu kipande cha Tunduma hadi Ikana utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 27 huku kazi ikiendelea na Ikana - Laela maendeleo ya kazi ji asilimia 41.24 ambapo miradi hiyo yenye urefu kilometa 64.2  kila mmoja inatarajia kukamilika june 30 mwakani.

Katika hatua nyingine, zaidi ya Sh bilioni 5 zimetengwa kwaajili ya matengenezo ya kawaida, maalumu na ukarabati ya barabara za mkoa wa Rukwa katika mwaka huu wa fedha wa 2012 na 2013. 

Alisema kuwa licha kutenga fedha hizo kwaajili ya kilometa 897.84 zitakazofanyiwa ukarabati pia madaraja zaidi ya 45 yatafanyiwa matengenezo ambapo kati ni maane makubwa.

Mhandisi Kabaka alisema kuwa bado changamoto nyingi zimekuwa zikijitokeza ambazo baadhi yake ni wizi wa vifaa vya ujenzi kama vile Mafuta, Saruji, Nondo na Vipuri hasa kwa wakandarasi wakuba hali inayosababisha kurudisha nyuma jitihada za Serikali katika kuharakisha maendeleo.

Blogzamikoa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa