Home » » WAZAZI WANACHANGIA WATOTO WA KIKE KUPATA MIMBA MASHULENI

WAZAZI WANACHANGIA WATOTO WA KIKE KUPATA MIMBA MASHULENI

Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu

Mwamko  mdogo wa  elimu miongoni wa wazazi na walezi katika wilayani ya Kalambo mkoani Rukwa, ni kichochea  cha watoto wengi wa kike kwenye shule za sekondari  kuacha  masomo kutokana na kupata ujauzito, imefahamika.

Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwimbi alipokuwa akimkaribisha kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Honest Mwanossa ili aweze kutoa ujumbe wa Mwenge huo.

Alisema kuwa katika muda mfupi aliokaa katika wilaya hiyo amebaini kuwa tatizo hilo ni kubwa miongoni mwa wazazi na walezi hali ambayo inadumaza maendeleo ya mkoa huo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa kutokana na  wazazi wengi kuwa mwamko mdogo wa kielimu wamekuwa kikubali watoto wao kuacha shule na kuwaoza ili wapate mali na kusahau kwamba wana haki ya kupata elimu ambayo ingeweza kuwasaidia katika maisha yao.

Alisema kuwa pia Serikali inapotaka kuwadhibiti wale waliowapa ujauzito wanafunzi baadhi ya wazazi, wamekuwa wakishirikiana na watu waliowapa mimba wanafunzi hao kwa kuwaficha na kuwatorosha kitu ambacho kinachangia ugumu wa kudhibiti tatizo hilo.

Chang'a aliwataka wazazi na walezi hao kubadilika kimtizamo na kifra na kujenga utamaduni wa kumsomesha mtoto wa kike kwani naye ana mchango mkubwa si tu kwenye familia lakini kwa ustawi wa taifa hili.

Alisema kuwa tatizo la mimba mashuleni linaweza kupungua iwapo wazazi wenyewe watakerwa na tatizo hilo, ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola pale wahusika wanaotenda makosa hayo wanapotiwa mikononi mwa sheria.

Naye Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, Honest Mwanossa alisema kwamba imefika wakati sasa watendaji wa Serikali kuhakikisha kwamba miradi inayotekelezwa iendane na thamani halisi ya fedha iliyotolewa tofauti na sasa ambapo miradi mingi imekuwa ya kiwango cha chini na haifanani na fedha halisi iliyotolewa na Serikali.

Blogzamikoa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa