Home » » UHAMISHWAJI HOLELA WA MIFUGO CHANZO CHA MAGONJWA.

UHAMISHWAJI HOLELA WA MIFUGO CHANZO CHA MAGONJWA.

Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Dk. Winston Mleche, akizungumza jana katika kikao kwaajili ya uanzishwaji wa eneo huru na magonjwa ya mifugo uliofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga, Wizara ya maendeleo ya mifugo na Uvuvi imeandaa mpango wa uanzishwaji eneo huru na magonjwa ya mifugo katika wilaya za Nkasi, Kalambo na Sumbawanga mkoani Rukwa. picha na Mussa Mwangoka.
 Mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano kwaajili ya uanzishwaji wa eneo huru na magonjwa ya mifugo, uliofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa. Picha na Mussa Mwangoka.
 
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa kina mada zinazotolewa katika mkutano kwaajili ya uanzishwaji wa eneo huru na magonjwa ya mifugo leo mjini Sumbawanga. Picha na Mussa Mwangoka.

Washriki wa mkutano wa kwajili ya uanzishwaji wa eneo huru na magonjwa ya mifugo kutoka mikoa zaidi 14 wakiwa katika picha ya pamoja leo mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo. Picha na Mussa Mwangoka. 
--------------------------------------------------- 
Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu

UHAMISHWAJI holela wa mifugo unaofanywa na baadhi ya wafugaji kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa ni miongoni mwa sababu zinazochangia sekta hiyo kushindwa kuzuia magonjwa ya mifugo nchini.

Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga, Moshi Chan'ga alisema hayo jana wakati akifungua Mkutano wa siku mbili wa kujadili uanzishwaji wa eneo huru na magonjwa ya mifugo, uliofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Alisema kuwa baadhi ya wafugaji wamekuwa wakitumia njia mbalimbali ikiwamo ya kutoa rushwa ili kuhakikisha wanahamisha mifugo yao kutoka eneo moja kwenda jingine hali ambayo imekuwa ikisababisha maafisa wa mifugo kutoa vibali bila kufuata utaratibu za kisheria.

"Nawajua wafugaji aina moja wasukuma.... wengine siwajui, msukuma yoyote anagawa kundi la ng'ombe katika makundi matatu kundi la kwanza ni la uzalishaji bila kujali watakavyozaliana, kundi la pili ni la huduma kwenye familia hili kazi yake ni kwenda kwenye minada na tatu ni baya kweli kweli hilo kundi la rushwa yaani msukuma amekwishandaa kabisa ng'ombe hawa akisha kamatwa atatoa ng'ombe" alisema.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo ndio maana baadhi ya maafisa mifugo wamekuwa wakikiuka sheria na kutoa vibali hovyo hovyo vya kuidhinisha ng'ombe waondoke hali inayosababisha kuwapo na ugumu katika kudhibiti magonjwa ya mifugo.

Aliwataka maafisa mifigo kubadilika kifikra na mitazamo na kuachana kuendekeza kupokea rushwa kutoka kwa wafugaji hali ambayo itasaidia kudhibiti usafirishwaji kihole wa mifugo ambayo insakuwa na magonjwa.

Chang'a aliongeza kuwa sekta ya mifugo ina uwezo mkubwa sana wa kuchangia kwenye pato la taifa ila bahati mbaya watu wafugaji wamekuwa wakinyanyaswa hata pale ambapo walitakiwa kuelimishwa lakini watu hawafanyi hivyo na hawataki kumjengea mfugaji mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kumsaidia kusafirisha mifugo yake kwa njia nzuri.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini, Dk. Winston Mleche, alisema kuwa wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi imeandaa mpango wa uanzishwaji wa eneo huru na magonjwa ya mifugo katika wilaya za Nkasi, Kalambo na Sumbawanga lengo na azma hiyo ni kuwezesha kufanyika kwa biashara ya mifugo na mazaoya mifugokwa kufuata vigezo na masharti ya kimataifa.
Blogzamikoa
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa