Home » » SAKATA LA BWAWA LA KAWA LAINGIA KATIKA SURA MPYA, MZINDAKAYA AITISHIA SERIKALI

SAKATA LA BWAWA LA KAWA LAINGIA KATIKA SURA MPYA, MZINDAKAYA AITISHIA SERIKALI


Waziri wa maji, Prof. Jumanne Maghembe kushoto akipewa maelekezo na Mhandisi wa maji wa wilaya ya Nkasi Mwaiyala Robert (katika) kushoto ni mwekezaji wa shamba la Nkundi lililopo bwawa la Kawa, Dk. Chrisant Mzindakaya. Picha na Mussa Mwangoka.  wa Rukwa yetu Blog



Mussa Mwangoka, Sumbawanga, Rukwa yetu Blog
SAKATA la mradi wa ujenzi wa bwawa la Kawa lililopo ndani ya Ranchi ya Nkundi iliyo chini mwakezaji mzalendo Dk. Chrisant Mzindakaya limechukua sura mpya baada ya mwekezaji huyo kutishia kuirejeshea Serikali fedha zake kiasi cha Sh. Bilioni 1.09 iliyotoa kwaajili ya ujenzi wa mradi.

Mwekezaji huyo alitoa kauli hiyo juzi mbele ya Waziri wa Maji, Prof Jumanne Maghembe aliyetembelea bwawa hilo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani Rukwa, ambapo Mzindakaya alisema kuwa yupo tayari kurejesha fedha hizo kwa Serikali iwapo ataendelea kupigiwa kelele zisizo na tija kutoka kwa wanasiasa.
"Nimewasiliana na benki yangu  ambayo nayo  imeafiki ,sasa kama kama mnataka niwarejeshee fedha zenu nipo tayari kufanya hivyo tuone tunamkomoa nani.....kati ya mimi na ninyi, wanasiasa wanapiga kelele tu wakati wananchi na Halmashauri ya wilaya ya Nkasi wako kimya wanaendelea kutekeleza mradi isitoshe kama nisinge anzisha mradi huu mgempigia nani kelele  hii ni  kwa  sababu  lipo " alisema Mzindakaya.
Aliongeza kuwa ili kuhakikisha maji yanayopatika katika bwawa hilo yanakuwa salama kwa matumizi ya wananchi wa vijiji watakaonufaika na mradi amelazimika kusitisha matumizi ya josho lake kwa  zaidi ya miaka mitatu ambalo lilikuwa na thamani Sh milioni 20.
Hata hivyo, Waziri Maghembe alisema kuwa kwa hali ilivyo hakuna sababu ya kuwapo kwa malumbano baina ya wanasiasa na mwekezaji huyo iwapo Serikali ngazi ya mkoa, Halmashauri na wananchi wameridhia mradi huo na kwamba jambo la msingi ni kuhakikisha vijiji husika vinapata maji.
Kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya bwawa hilo ulioanza kujengwa Desemba 2008 kwa gharama ya zaidi bilioni moja na mkandarasi Nyakirang'ani Construction Ltd utawanufaisha wakazi wa vijiji vya Nkundi, Fyengerezya na Kalundi, vilivyopo wilayani Nkasi, mkoani Rukwa.
Hata hivyo Mzindakaya ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya SAAFI Ltd inayomiliki shamba hilo na kiwanda cha kusindika nyama ameingia katika mvutano mkubwa na Mbunge wa Nkasi Kaskazini Ally Keissy ambaye hivi karibuni amekaririwa na vyombo vya habari akilaani ufujaji fedha hizo  za umma zilizotumika kujenga mradi huo kwa kile kilichoelezwa ni kwa“manufaa ya familia ya mtu mmoja.”

Keissy alidai fedha zilizotumika katika mradi huo uliojengwa kwenye shamba la mifugo la Mzindakaya, zingeweza kujenga visima 80 virefu, ambavyo vingesaidia wananchi wa vijiji hivyo kupata maji ya kutosha.

Naye Mkurugenzi  Msaidizi wa Wizara ya Maji Frida Rweyemamu alisema kuwa kwa mwaka huu wa fedha Serikali imetenga Sh milioni 300 kwaajili ya kuendelea na ujenzi katika bwawa hilo lenye uwezo wa kuhifadhi lita za ujazo 546000 za maji.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa