Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa yetu
MKUU wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Moshi Chang’a amesema vitendo vya ubinafsi, rushwa na ufisadi kwa baadhi ya maofisa Serikalini kimekuwa kichochea kikubwa cha ujenzi holela katika mijini hapa nchini jambo ambalo linaloigharimu Serikali kwa kutumia fedha nyingi katika kulipa fidia wananchi wanapotakiwa kuondoka katika maeneo hayo.
Chang’a alisema hayo kwa nyakati tofauti katika ziara yake iliyoanza juzi ya kutembelea Kata zote 17 zilizopo wilayani humo yenye lengo la kujitambulisha, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kusalimiana na wananachi.
Alisema kuwa kutokana na makazi ya wakazi wengi kujengwa kiholela katika miji mingi nchini Serikali italazimika kutumia fedha nyingi kuwalipa fidia ili waweze kupisha ujenzi wa huduma muhimu kama barabara, masoko, sehemu za ibada na nyinginezo.
Hivyo, aliwaagiza viongozi wilayani humo kuhakikisha wanawashirikisha wadau wote wa maendeleo katika kazi ya upangaji wa mji wa Matai ambayo ni makao makuu ya wilaya hiyo ya Kalambo.
“Kuna uzembe unaofanywa na baadhi ya watendaji Serikalini ambao wamekuwa wakifumbia macho ujenzi holela kwenye baadhi ya miji hapa nchini, hali inayosababisha kuvurugika kwa mipango miji, nitawashughulikia sawasawa” alisema Chang’a.
0 comments:
Post a Comment