Home » » Majambazi yaua wawili Rukwa

Majambazi yaua wawili Rukwa



Mussa Mwangoka-Rukwa yetu

JESHI la polisi mkoani Rukwa linashikilia watu wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la mauaji ya wafanyabiashara wawili na kupora mamilioni katika kijiji cha Kaengesa wilayani Sumbawanga.

Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa Jacob Mwaruanda alisema jana ya simu kuwa tukio hilo lilitokea alfariji kuamika jana ambapo kundi la watu hao hao walifanya mauaji kwa nyakati tofauti katika eneo la Kaengesa na kijiji cha Lula.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana zinadai kuwa kati ya watu wawili waliokufa mmoja ndiye alitambuliwa kuwa ni Abineli Kasonje mkazi wa Lula ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na kumjeruhi mke wake kwa panga wakati mabishano ya kulazimishwa awape pikipiki yake ili watoroke nayo.

Mwaruanda alisema kuwa kabla ya kuvamia nyumba ya Kasonje na kumuua, awali waliiteka kwa muda mfupi nyumba moja ya kulala wageni iliyopo eneo la Kaengesa ambapo waliingia chumba kimoja hadi kingine ambako waliwalazimisha wageni waliokuwa wamelala katika vyumba hivyo kutoa fedha, simu na vingine vya thamani sambamba na kuwachapa na viboko.

Kamanda Mwaruanda alisema kuwa wakati wakiendesha operesheni hiyo watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walimpiga risasi na kumuua mfanyabiasha mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja ambaye inaelezwa alifika kijijini hapo kwaajili ya kununua mazao ya mahindi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo mfanyabiashara huyo anadaiwa kutoka mji mdogo wa Mlowo wilayani Mbozi mkoani Mbeya ambaye aliiuawa kwa kupigwa risasi iliyopata kifuani na kufariki dunia akiwa chumbani baada ya kukosa msaada wa aina yoyote.

Hata hivyo kufuatia kusikika kwa milio ya risasi na kelele za watu walijitokeza wasamaria wema ambapo iliwabidi majambazi hao kukimbia na kuelekea kitongoji cha jirani cha Lula na kuvamia nyumba ya Kasonje ambako walimuua mtu huyo.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, baada ya polisi kupata taarifa hiyo walifanya msako ambapo walifanikiwa kuwanasa watuhumiwa wawili ambao majina yao yanahifadhiwa walionanaswa katika kijiji cha Msanzi umbali wa  zaidi ya kilometa 20 kutoka eneo la tukio.

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa