.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akiwapokea wageni hao katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga mara baada ya kushuka kwenye ndege hiyo.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa akiendelea na ukaribisho wa wageni hao. Jumla ya wawakilishi hao walikuwa nane ambao ni Clement Mndesha (Beach Petroleum Tanzania LTD), Marcus J. Mng'ong'o (Beach Petrolleum Tanzania LTD), Sebastian Shana (TPDC Dar es Salaam), Elias Kilembe (TPDC Dar es Salaam), Raffaele Fantini (Furgo Oceanismica Rome Italy), Mike Mc ulemanin (South Afica), Danny Burus (Beach Energy Australia), na Ban De Swamsa (Omega Security).
Picha zaidi Bofya Hapa
Wawakilishi wa Kampuni ya Beach Petroleum na Shirika la TPDC Tanzania ambao ni wabia wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga na ndege ya shirika la Tanzaniair hivi karibuni kwa ajili ya kuonana na uongozi wa Mkoa wa Rukwa kujadili mradi wa uzalishaji wa mafuta ya Petroli na Gesi inayokadiriwa kuwepo Mkoani Rukwa hususani katika kingo wa Ziwa Tanganyika, mkandarasi wa kazi hiyo ya utafiti ni Furgo Oceanismica ya Rome Italy.
Kwa Mujibu wa wawekezaji hao mategemeo waliyokuwa nayo hadi hivi sasa ni kufanya utafiti wa kina juu ya eneo linalokadiriwa kupatikana mafuta ya Petroli na Gesi kwa lengo la kuainisha eneo maalum kwa ajili ya uchimbaji nishati hizo. Kazi hiyo inategemewa kuanza mapema mwezi huu (Aprili 2012) na itakamilika katika kipindi cha miezi mitatu ijayo. Pindi kazi hiyo itakapokamilika kibali maalumu kutoka EWURA kwa ajili ya kuruhusu zoezi hilola uzalishaji wa mafuta kitahitajika ili kazi ianze mara moja.
Hata hivyo kuna changamoto ambazo wanakabiliana nazo ambazo ni kibali cha kuweza kutumia Ukanda wa Ziwa katika upande wa nchi jirani ya Kongo ambapo Meli zitakazokuwa zikifanya kazi kwenye mradi huo zitalazimika kutumia eneo hilo kama sehemu ya kutafutia mzunguko (Turning Point) na kurudi Ukanda wa Tanzania. Eneo la upande wa Nchi ya DRC Kongo litakalotumika ni kati ya K.m 1.5 hadi K.m 3 majini.
Changamoto nyingine ni kukosekana msaada kutoka ubalozi wa Kongo uliopo Dar es Salaam, hii ikiwa ni pamoja na kutopata majibu ya barua na Emails zilizopelekwa kwao kwa ajili ya kufuatilia uwezekano wa kutumia Ukanda wa Ziwa wa Nchi hiyo kwa ajili ya mapitio ya Meli wakati wa utekelezaji wa mradi huo.
Yapo maombi ambayo Wawekezaji hao waliyatoa kwa Mkoa wa Rukwa ambayo ni:
Mkoa usaidie mawasiliano na wenzi wao wa Nchi jirani ya Kongo kuweza kupata uelewa wa mradi huu kuepusha usumbufu wowote wa kiusalama.Elimu na taarifa ziwafikie wananchi wakiwemo wavuvi na wanakijiji wapate elewa juu ya shughuli zote za mradi huo waweze kutoa ushirikiano na kuepusha usumbufu wowote.
Usalama wakati wote wa zoezi hilo la utafiti na uchimbaji wa rasilimali hizo.
Kufanyike mawasiliano baina ya Beach Petroleum, TPDC na Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa. Mkoa usaidie Mtaalamu wa uvuvi ambaye atashirikiana na Wataalamu katika meli wakati wa utafiti
Picha zaidi Bofya Hapa
0 comments:
Post a Comment