Home » » 36 WAITWA MAHAKAMANI MAHUDHURIO YA WATOTO.

36 WAITWA MAHAKAMANI MAHUDHURIO YA WATOTO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


WAZAZI 36 wamesaini hati ya kuitwa kwenye shauri Mahakama ya Mwanzo Mji mdogo wa Chala wilayani Nkasi, Rukwa kwa kutowapeleka shule watoto wao waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza, Januari mwaka huu.
Akizungumza na gazeti hili Hakimu wa mahakama hiyo, Wilgis Mbunda alisema wazazi hao wameitwa mahakamani hapo baada ya ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Mkwamba wilayani humo kuwasilisha majina 39 ya watoto ambao hawajaripoti katika shule ya sekondari Mkwamba bila taarifa yoyote.
Alisema Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo alipokea taarifa hiyo kutoka kwa mkuu wa shule hiyo ambapo alisema kabla ya kufikia hatua hiyo ofisi ya kata iliwaita wazazi hao ili kujua sababu za watoto wao kutofika shuleni lakini hawakutoa ushirikiano wowote.
“Ndipo Ofisa Mtendaji huyo alipofika mahakamani na Mahakama imeamua kuwapelekea hati ya mwito mahakamani wazazi hao ili sheria iweze kuchukua mkondo wake,” alisema.
Hakimu Mbunda alisema kuwa wazazi hao watashtakiwa kwa kifungu cha sheria za kanuni ya elimu namba 3 mwaka 2005.
CHANZO: HABARI LEO
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa