Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe,
amewataka wanafunzi wa kidato cha sita kujitokeza kwa wingi na kupiga
kura katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu, ili kumchagua kiongozi
atakayewafaa.
Chikawe alitoa ushauri huo kwenye mahafali ya nne ya kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya St. Cathedral.
Chikawe alisema watakapojiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura, itawasaidia kumpigia kura kiongozi wanayemtaka.
“Usipojiandikisha kupiga kura utaishia kulalamika kuwa kiongozi
huyu hafai, ila ukijitokeza kwenye uchaguzi na kupiga kura, utamchagua
kiongozi unayemtaka na atakaye kufaa,” alisema Chikawe.
Pia, aliwataka wahitimu hao kujiepusha makundi ya kihalifu ukiwamo ugaidi ambayo yanaweza kuchafua sifa zao.
“Dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kigaidi, naomba
msijihusishe wala kushiriki katika vitendo hivyo ambavyo vinaweza
kuwaingiza kwenye makundi yasiyofaa na kuharibu sifa zenu,” alisema.
Naye Mkuu wa shule hiyo, Sister Theodora Faustine, alimshukuru
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali
Pengo, kwa kuwasiadia kuwapa shule hiyo.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment