Home » » GARI LA ASKARI LAUA MTEMBEA KWA MIGUU

GARI LA ASKARI LAUA MTEMBEA KWA MIGUU

 MTU mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya gari kuacha njia na kuwagonga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isunto Mantage, alisema jana kuwa ajali hiyo ilitokea juzi, saa 2.30 usiku katika Kitongoji cha Kakunku, kilichopo Kata ya Utende, wilayani Mpanda.

Alisema gari aina ya Toyota Mark II namba T 748 AAF, mali ya askari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mpanda, lililokuwa likiendeshwa na askari E 8834 Ephraim, liliwagonga watembea kwa miguu hao na kusababisha kifo cha mmoja wao.

Alimtaja aliyegongwa na kufariki dunia kuwa ni Lumondya Mwandu (50), mkazi wa Tarafa ya Karema, aliyekuwa amekwenda katika kijiji hicho kuhudhuria mazishi ya ndugu yake.

Aliyejeruhiwa katika ajali hiyo ni Jilala Lufunga (32), mkazi wa Kijiji cha Mgombe. Amevunjika mguu wake wa kulia na amelazwa katika Kituo cha Afya cha Ingongwa.

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana. Polisi bado wanaendelea na uchunguzi.

 Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa