Na Walter Mguluchuma
Sumbawanga
Taasisi moja siyo ya kiserikali mkoani Rukwa CEELS
linalojishughulisha na uboreshaji wa huduma za kiuchumi za kijamii na msaada wa
kisheria limetoa ushauri kwa viongozi wa serikali wilayani Kalambo mkoani Rukwa
kuimarisha utoaji wa elimu sahihi ya uzazi wa mpango ili uwezo wa kiuchumi wa kila kaya ulingane na ukubwa wa
idadi ya watu katika familia moja
Mratibu wa kitengo cha utafiti cha Taasisi hiyo Willian
Nathan alitoa kauli hiyo wakati wakilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa
Afrika iliyofanyika kiwilaya hivi karibuni kwenye kiijiji cha Kisumba ya watoto
kilichopo kata ya Kisumba ili kutekeleza kauli mbiu isemayo boresha uzalishaji
na usalama wa chakula kwa lishe bora
ALISEMA utafiti uliozihusisha kaya za wananchi wanaoishi
katika vijiji 9 vinavyounda kata ya
Kisumba umegundua kuwa uzalishaji wa mazao ya chakula na pia njia mbalimbali za
kujipatia kipato cha kila kaya hakilingani na idadi ya watu wanaounda familia
moja hali aliyosema inazorotesha afya za wanafamilia na kuishi katika hali ya
umaskini
Nathan alisema CEELS iliamua kuwa na wiki ya
maadhimisho ya kilele cha siku ya mtoto wa Afrika kwenye kijiji cha Kisumba
kutokana na utafiti unaodhihirisha kuwapo kwa kasi kubwa ya uzazi katika kijiji
hicho na vingine 8 vinavyounda kata hiyo ikilinganishwa na maeneo mengine ya
vijiji vya wilaya hiyo ya Kalambo
Alisema serikali kwa kushirikiana na wadau wengine katika
sekta ya afya inatakiwa kuwa na mpango mkakati endelevu wa kuhakikisha kila
familia inakuwa na mpango wake madhubuti wa kuwa na idadi stahili ya watoto kwa
kuzingatia uwezo wake wa kiuchumi badala ya kuwa na idadi kubwa ya watoto
wanaokuwa mzigo katika malezi na kukosa huduma muhimu za kijamii ambazo ni
pamoja na elimu mavazi na huduma nyingine za afya
Mmoja wa waelimisharika wa CEELS aliyeshiriki kutoa mafunzo
ya jinsi ya jinsi ya kuboresha uzalishaji wa vyakula Happyness Dawson alisema
baadhi ya wanachi katika vijiji hivyo vya kata ya Kisumba wanashindwa kuwa na
mpango mzuri wa lishe bora kutokana na kiasi kidogo cha mazao ya chakula inayozalishwa
ikilinganishwa na idadi kubwa ya watu
katika familia moja
Alisema kutokana na hali hiyo ya watoto wengi wenye umri wa
chini ya miaka mitano hupata magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na utapiamlo napia kusababisha afya ya mama na
baba kutokuwa imara kwa kukosa lishe bora kutokana na uzazi wa karibu kila
mwaka unaowafanya washindwe kupanga mipango sahihi ya huduma za afya na pia
elimu kwa watoto wao
Afisa mtendaji wa kata hiyo Nelly Gervas alisema katika taarifa
yake katika kwenye maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa Afrika kuwa vijiji 9
vya kata ya Kisumba vya Kapozwa Mpombwe Ngorotwa Nondo Kisumba Kasote Chisenga
Kafukoka na Kachele vina jumla ya watoto chini ya umri wa miaka mitano zaidi ya
98 elfu ikilinganishwa na idadi ya watu wazima kiasi cha elfu 23
Alieleza ndio maana hata jina la kijiji cha Kisumba
limebadilika na kuitwa na watu mbalimbali kuwa Kisumba ya watoto kutokana na
idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa bila kuzingatia uwezo sahihi wa kila kaya
ambapo alisema kwa wastani familia yenye kuwa na idadi ndogo ya watoto huwa ni
watoto watano
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment