Home »
» DR CHRISTIAN MZINDAKAYA ANYANG'ANYWA NYUMBA 12 ZA UMMA AMBAZO ALIKUWA AMEZIPANGA KIBIASHARA KWA MIAKA 12.
DR CHRISTIAN MZINDAKAYA ANYANG'ANYWA NYUMBA 12 ZA UMMA AMBAZO ALIKUWA AMEZIPANGA KIBIASHARA KWA MIAKA 12.
Jiunge na Huduma ya Tone Mobile News Bure kabisa kupitia Whatsapp yako na uwe wa kwanza kupata kile kinachotokea ni Rahisi sana Ingia katika uwanja wa kuandika ujumbe mfupi wa maneno katika Whatsapp yako kisha andika TONE MOBILE NEWS tuma kwenye namba 0756364660 utapokea ujumbe kuwa umeunganishwa.
Walter Mguluchuma Sumbawanga .- Rukwa yetu
HATIMAYE wizara ya Ujenzi imeinyang’anya Kampuni ya Agriculture and Animal Food Industries Ltd (SAAFI) iliyomilikiwa na mwekezaji mzalendo,na mwanasiasa mkongwe , Dk Chrisant Mzindakaya nyumba 12 za umma Serikali ambazo alikuwaamezipanga kibiashara kwa miaka 12 .
Nyumba hizo ambapo 11 za kuishi na moja ikiwa ni ofisi zilijengwa na Shirika la Maendeleo la nchini Norway mwaka 1988 zimekabidhiwa rasmi Juni 17 , mwaka huu, kwa Wakala wa Majengo (TBA) mkoani hapa na Wizara ya Ujenzi .
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi huo wa Serikali baada ya kukagua nyumba hizo jana , Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), Aish Hilaly alisema :- “ Leo nina furaha kubwa sana kwani nyumba hizi zilikuwa zikininyima usingizi kutokana na maofisa serikalini wakimwemo majaji na baadhi ya wakuu wa idara kuishi katika nyumba za kupanga lakini sasa wataishi katika nyumba hizi ambazo ni bora zenye ulinzi mzuri na usalama wa kutosha “ alibainisha .
Nyumba maarufu kama ‘compound ‘ limejengwa katika eneo la Mkoani katika Mji wa Sumbawanga .
Alibainisha kuwa baada ya kutembelea nyumba hizo na kuzikagua akiongozana na Meneja wa Wakala wa Majengo mkoa wa Rukwa , Deocles Kalikawe amebaini kuwepo kwa mapungufu makubwa akidai kuwa mwekezaji aliyezipanga kibiashara atalipia gharama zote za ukarabati .
“Nampongeza Waziri wa Ujenzi , Dr John Pombe Magufuli kwa maamuzi magumu aliyoyafanya ya kuzirejesha nyumba hizi Serikalini kupitia TAB…… nimemshauri Meneja wa TBA mkoani hapa moja ya nyumba hizi iwe kwa ajili ya kufikia viongozi wa kitaifa kwani iliweahi kutokea tulifikiwa na wageni wawili kutoka taifani mmoja alilala Ikulu ndogo lakini mwingine alilazimika kulala hotelini “ alisisitiza
Nae Meneja wa TBA mkoani hapa , Kalikawe alieleza kuwa mara baada ya kukabidhiwa rasmi nyumba hizo waliwamua kuweka walinzi wao wakati wakijipanga kufanya tathmini ya ukarabati wa nyumba hizo ili ziweze kupangishwa kwa majaji na watumishi wa mahakama pia wakuu wa idara .
Alibainisha kuwa kati ya nyumba hizo tatu ni za daraja A zenye vyumba vitano , tatu zingine nazo ni daraja A lakini zina vyumba vinne na nyumba tano daraja B zikiwa na vyumba viwili .
Wakazi wa mjini hapa waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi wameipongeza Serikali kwa kuchukua uamuzi huo kwamba utapunguza tatizo la uhaba wa nyumba kwa maofisa Serikalini .
“Tatizo la uhaba wa nyumba ni changamoto kubwa sana mkoani hapa ambapo imesababisha baadhi ya watumishi wanaopangiwa kuja kufanya kazi huku kukataa kuja kuripoti au wanafika na kuripoti lakini wakiondoka hawarfudi tena …” anasema Enos Budodi mkazi wa mjini hapa .
Nae Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na shughuli za kijamii na maendeleo (UDESO kwa mikoa ya Rukwa na Katavi, Eden Wayimba alieleza kuwa kurejeshwa Serikali kujireshea mali yake yenyewe kutawapunguzia gharama za maisha watumishi wa umma watakaopangishwa .
Kurejeshwa kwa nyumba hizo, ni ushindi mkubwa kwa Aeshi ambaye tangu awali amekuwa hana mahusiano mazuri ya kisiasa na Dk. Mzindakaya ambapo mara kadhaa mbunge huyo alikuwa akihoji uhalali ya nyumba hizo kumilikiwa na kampuni ya mtu binafsi badala ya kutumia na watumishi wa Serikali.
Lakini wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanadai kwa uamuzi huo utaongeza chuki ya kisiasa kati ya wanasiasa hao wawili mahasimu ambao mara ya mwisho walikutana mwezi meikwenye ibada ya kusimikwa kwa askofu wa kanisa Moravian jimbo la Rukwa, Cornad Nguvumali.
Ibada hiyo ilifanyika kwenye uwanja wa michezo wa Nelson Mandela uliopo mjini hapa ambapo mkuu wa mkoa aliwataka wazike tofauti zao lakini Dk. Mzindakaya alikataa kumsamehe Aeshi kwa madai hakuandaliwa kiroho kutoa msahama kwenye ibada hiyo.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
0 comments:
Post a Comment