Home » » DED ATANGAZA KIAMA

DED ATANGAZA KIAMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa, Julius Kaondo, amewapiga marufuku walimu wa shule za msingi na sekondari kuwafanyisha kazi ngumu na kwenye jua kali wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi.

Akizungumza juzi wakati akizindua kituo maalumu cha upimaji wa kielimu kilichoko katika Shule ya Msingi Nkomolo, Kaondo alisema kitendo hicho kinahatarisha afya za wanafunzi hao, hivyo kuwaweka katika mazingira yanayoweza kufupisha maisha yao.

Alisema watu wenye matatizo ya ulemavu wa ngozi, hawapaswi kukaa katika mionzi mikali ya jua kwa kuwa inawasababishia ngozi kupata saratani.


Kutokana na hali hiyo, alisema ni busara kuwachukulia kuwa ni watu maalum na wanahitaji uangalizi maalum, ili kuwakinga na maradhi mbalimbali yanayoweza kuwakumba ikiwamo saratani ya ngozi.

Kaondo pia aliwataka wanafunzi wote wenye ualbino kutumia mafuta maalum wanayopewa kama msaada au kuyanunua, ili kuzuia mionzi ya jua kwa sababu baadhi yao wamekuwa hawayatumii kwa kukosa elimu sahihi, hivyo kujikuta wakisumbuliwa na matatizo ya ngozi. 

Mkurugenzi huyo, alisema baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa aina tofauti, wakati mwingine wao wenyewe wamekuwa hawajijali hata wanaposaidiwa na wahisani na kwamba hiyo inatokana na kutokuwa na elimu ya kutosha au kujikatia tamaa.

Awali, Mkurugenzi wa Mradi huo, unaojulikana kama International Aid Service (IAS), Irene Shayo, alisema mradi huo unafadhiliwa na Denmark kwa ushirikiano na Kanisa la Free Pentecostal la Tanzania (FPCT).

Shayo aliwasihi watu wenye ulemavu wa ngozi na wa aina nyingine kujijali na kujipenda kwa kuwa pamoja na changamoto walizo nazo, wanaweza kufanya mambo makubwa ambayo hata wasio walemavu wanashindwa, hivyo wanatakiwa kupambana bila kukata tamaa. 

Chanzo:Nipashe
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa