Home » » MGANGA WA JADI ACHOMWA MKUKI MGONGONI

MGANGA WA JADI ACHOMWA MKUKI MGONGONI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Imeandikwa na Peti Siyame, Sumbawanga
WATU watano wakiwemo watoto wawili wamekufa katika matukio tofauti yaliyotokea mkoani hapa hivi karibuni ambapo mganga wa jadi, Levocatus Kanjalanga (65) aliuawa kikatili kwa kuchomwa mkuki mgongoni na mtu asiyefahamika.
Matukio hayo ambayo yametokea katika Wilaya za Nkasi, Kalambo na Manispaa ya Sumbawanga yamethibitishwa kwa nyakati tofauti na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando (pichani) na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Said Mtanda.
Mtoto wa mganga huyo, Simon Kanjalanga alilieleza gazeti hili kuwa baba yake aliuawa juzi saa moja na nusu asubuhi kwa kupigwa na mkuki mgongoni akiwa anatembea mitaani katika kitongoji cha Chawe kilichopo katika Mji wa Namanyere wilayani Nkasi.
Taarifa kutoka eneo hilo la tukio zinaeleza kuwa mganga huyo wa kienyeji alikuwa akituhumiwa na wateja wake kuwa alikuwa akiwatoza fedha nyingi za matibabu lakini walikuwa hawaponi kupitia uganga wake huo.
Akithibitisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Mtanda alieleza kuwa watu wawili wameuawa kikatili wilayani humo akiwemo mganga huyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina .
CHANZO HABARI LEO
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Rukwa Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa